Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

BaTumtQhYGb.jpg
 

Hapana. Mimi siyo Linguist...
Napenda tu mambo ya kitamaduni - lugha, mila na tamaduni zetu wenyewe kwa ujumla.
Aliyeandika hiyo kamusi simkumbuki lakini ni Mjapani kabisa wala siyo Mswahili.

Wajapan na Wajerumani wanaandika vitabu vingi vya lugha zetu. Chuo Kimoja kule Japan kuna Taasisi kabisa inayojishughulisha na utamaduni wa Kiafrika na wamechapisha kamusi za makabila mengi ya Tanzania. Kuna mwanafunzi wa uzamifu kutoka Japan anaandika kamusi ya Kisukuma na huwa namsaidia mara kwa mara. Kuna Profesa mmoja kutoka Chuo Kikuu cha Ohio pia ameandika mambo mengi sana kuhusu Kikerewe.

Wanafunzi wa Kiswahili huko Leipzig University sasa wanaweza kuandika dissertations zao kwa Kiswahili safi kabisa mpaka unashangaa. Kila kitu wanachofanya jamaa wapo siriazi sana !!!​

Hongera sana aisee. Kiswahili kinaendelea kukua kidogo kidogo! Mpaka tunandikiwa kamusi za lugha ya makabila yetu, jamaa wako serious sana! Swali la kichokozi kwako, je unaongea lugha ngapi kwa ufasaha kabisa?
 
Hongera sana aisee. Kiswahili kinaendelea kukua kidogo kidogo! Mpaka tunandikiwa kamusi za lugha ya makabila yetu, jamaa wako serious sana! Swali la kichokozi kwako, je unaongea lugha ngapi kwa ufasaha kabisa?
Cha kushangaza ni kwamba sina kipaji cha kujifunza lugha. Huwa sipendi kabisa lugha zenye gender na inflections ambazo ziko complicated. Nimejaribu lugha nyingi lakini karibu zote zinaniwia ngumu naishia tu kujua salamu na mambo machache ya muhimu.

Lugha tunazichukulia poa lakini kujifunza lugha mpya ni mojawapo ya njia bora kabisa ya kuimarisha afya ya ubongo.
Sasa hapa nilipo nahangaika na Kihispania...

Nimejibu swali lako kama mwanasiasa ha ha haaaa !!!​
 
Back
Top Bottom