Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

JINSI YA KUCHAGUA DAWA NZURI KWA KIKOHOZI NA MAFUA

Kikohozi na mafua ni miongoni mwa matatizo ya kiafya ambayo yapo kila siku katika jamii yetu. Hakuna siku hata moja ambayo hospitali au famasi itakosa mgonjwa wa kikohozi au mafua.
 
Kwa mfano wengi sana hufika famasi na kusema wanataka dawa za mafua za chenga chenga (Nyakati nyingine huwa nacheka na kujiuliza kama wanadhani chenga chenga ndo zinatibu vizuri mafua au hudhani kwamba dawa hizo husaidia kutibu mafua ya aina zote)

Sasa ni njia gani nzuri ya kuchagua dawa za kikohozi na mafua?
 
VITU VINAVYOSABABISHA MAFUA

Mafua hutokana na kuzalishwa kwa wingi zaidi kwa ute (mucus) katika sehemu za juu za mfumo wa upumuaji(puani). Yanaweza kuwa mengi zaidi na mepesi kiasi cha kuweza kutiririka au kuwa machache na mazito kiasi cha kuweza kuziba pua.
 
Miongoni mwa vitu vinavyoweza kusababisha mafua ni pamoja na

Maambukizi ya vijidudu vya magonjwa hususan virusi (Virusi vya mafua)
Mabadiliko ya hali ya hewa na kuwa na baridi au unyevu zaidi
Mzio (Aleji) kutokana na baadhi ya vitu kama vile vumbi, vipodozi, rangi nk
Ulaji wa pilipili nyingi
 
JINSI YA KUCHAGUA DAWA

Hakuna dawa moja ambayo inafaa kwa mafua na vikohozi aina zote au vinavyotokana na sababu mbalimbali. Kitu kizuri zaidi kufanya ni kujua chanzo cha mafua au kikohozi chako na kisha kutumia dawa inayofaa zaidi kwa mafua au kikohozi hicho
 
Njia rahisi zaidi ya kufanya hivyo na kufanikiwa vizuri ni kujieleza vizuri kwa daktari au mfamasia kisha atakushauri dawa nzuri zaidi kwako. Kuna uhusiano mkubwa sana kati ya kikohozi au mafua na matatizo mengine ambayo unaweza ukawa huyajui, kwa hiyo ni bora kumuelezea daktari au mfamasia jinsi unavyojisikia na kumuelezea chanzo cha tatizo lako (kama hukumbuki mwambie hukumbuki sababu au chanzo chake) ili yeye atafakari zaidi na kukushauri vizuri.
 
Back
Top Bottom