Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

b25c4ec230e911e43ecb8654f2964031.jpg
 
BARCA WANATAKA KUONDOA WATATU JANUARI


Barcelona itauza wachezaji kadhaa majira ya badiri kabla ya kusajili mtu yeyote, kwa mujibu wa Sport .
Miongoni mwa wachezaji ambao klabu hiyo ipo tayari kuwaruhusu kuondoka ni Aleix Vidal, Andre Gomes, Denis Suarez, Gerard Deulofeu, Arda Turan na Paco Alcacer.
 
KAKA KUCHEZA CHINA


Nyota wa Kibrazili Kaka atakuwa amemaliza kazi yake MLS, lakini inaonekana bado hajamaliza kucheza soka.
Corriere dello Sport limeripoti kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35 atasaini mkataba wa mwaka mmoja na klabu ya Ligi Kuu ya China Guizhou Hengfeng F.C.
 
REAL IMEKATAA OFA YA £40M YA BENZEMA KUTOKA ARSENAL


Ofa ya Arsenal ya paundi milioni 40 kwa ajili ya mshambuliaji wa Real Madrid Karim Benzema imekataliwa na klabu hiyo ya Hispania, kwa mujibu wa habari kutoka Diario Gol.
Bosi wa Gunners Arsene Wenger amekuwa akimkubali kwa muda mrefu mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa na klabu hiyo ya London inataka kutumia upenyo wa rais wa Real Florentino Perez kutaka kumuuza.
 
BARCELONA KUACHANA NA MPANGO WA KUMSAJILI OZIL


Barcelona bado wanasita kuhusu kumsajili mchezaji wa Arsenal, Mesut Ozil, wanawaza bado kama wamsajili au waache, kwa mujibu wa Sport .
Klabu hiyo ya Catalan imekuwa ikimfuatilia nyota huyo wa Gunners kwani mkataba wake na klabu hiyo ya London Kaskazini unakaribia kufika mwisho, lakini wanahofu jinsi anavyoishi kwani anaweza kuathiri ufanisi dimbani.
 
REAL MADRID WANAMTAKA RABIOT WA PSG


Real Madrid wanamtaka kiungo wa PSG Adrien Rabiot kuwa mrithi wa kudumu wa Luka Modric, kwa mujibu wa Don Balon .
Madrid tayari wameanza kutafuta mrithi wa Modric Santiago Bernabeu, na mchezaji huyo wa kimataifa wa Croatia atakuwa ametimiza miaka 33 mwaka ujao. Rabiot ni miongoni mwa wachezaji wanaomvutia Florentino Perez, sambamba na mshambuliaji wa Tottenham Dele Alli.
 
PSG YAMFUKUZIA FELLAINI


Paris Saint-Germain wanataka kumsajili Marouane Fellaini kutoka Manchester United mwisho wa msimu huu, Le 10 Sport limeripoti.
Timu hiyo ya Unai Emery inataka msaidizi wa Thiago Motta kwenye safu ya kiungo na wanaamini fiziki ya Mbelgiji huyo ni suluhisho sahihi.
 
Back
Top Bottom