Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

IMG-20171212-WA0004.jpg
 
Kinga ya awali (Primary Prevention)
Kuboresha huduma za afya na kijamii ili kuondoa tatizo la utapia mlo, kuongeza uhamasishaji, kuondoa tatizo la kuzaa watoto njiti, na kutoa elimu kwa kina mama wajawazito juu ya madhara ya madawa ya kulevya, unywaji pombe, magonjwa ya zinaa na nk wakati wa ujauzito
 
Kuboresha huduma za afya za kina mama, tiba ya magonjwa mbalimbali ili kuzuia maambukizi, ajali (trauma), madhara mbalimbali wakati wa ujauzito, kifafa cha mimba, na magonjwa ambayo yanaweza kumuathiri mtoto kabla, wakati na baada ya kuzaliwa.
 
Mtoto kupata chanjo dhidhi ya ugonjwa wa kifua kikuu, ugonjwa wa polio, ugonjwa wa surua na nk.
Kuwaelimisha kina mama wajawazito juu ya madhara ya madawa ya kulevya na umuhimu wa kuhudhuria kliniki
 
Kutoa ushauri nasaha kwa wazazi ambao wanaathari za viashiria vya asili (genetic counseling to high risk group)
Kufanya tafiti juu ya sababu au vyanzo vya upungufu wa akili pamoja na tiba yake.
 
Kuwaelimisha mama wajawazito jinsi ya kujifungua salama na umuhimu wa kuwasikiliza wahudumu wa afya wakati wa kujifungua kwani mara nyingi kina mama huwakosesha watoto wao hewa na hivyo kuwaweka katika hatari ya kupata upungufu wa akili na ndio sababu wahudumu wa afya wanakuwa wakali sana kwa kina mama wanaofanya hivyo kuchelea mama asipate mtoto mwenye tatizo hili. Hii itasaidia kuondokana na ile dhana ya kwamba kujifungua hospitali za serikali kwa mama mjamzito ni adhabu kwani huwa wanapigwa.
 
Kinga ya baadae (Secondary Prevention)
Ugunduzi wa mapema na tiba sahihi kwa matatizo yanayoweza kuzuilika kama phenylketonuria, hypothyroidism nk.
Ugunduzi wa mapema wa matatizo katika mfumo wa fahamu, mabadiliko ya tabia na hisia ili kukabiliana nayo mapema.
 
Back
Top Bottom