Baadhi ya magonjwa kama vile kisukari na magonjwa ya homoni (thyroid diseases).
Magonjwa haya huingiliana na mfumo wa mwili na pia huathiri afya ya ngozi.
Umri mkubwa
Kwa kawaida mtu anapokuwa na umri mkubwa sana, hata utendaji kazi wa mifumo mbalimbali katika mwili wake hupungua kiufanisi, hivyo hata kinga ya mwili pamoja na afya ya ngozi pia hupungua.
Mtu kutozingatia usafi wa miguu yake kwa kiwango kinacho stahili
Moja ya madhara yanayoweza kutokea kwa mtu kupasuka visigino ni kupata maambukizi ya magonjwa, infection. Hii ni endapo miguu itachanika kiwango cha kufikia ngazi ya kati ya ngozi, dermis, na kupelekea damu zianze kutoka sambamba na maumivu makali. Kupitia hiyo mipasuko mtu anaweza kupata maambukizi ya magonjwa.
Kwa miguu iliyopasuka tayari, ifanyie usafi miguu yako na kisha tumia mafuta ya mzaituni kupaka katika mipasuko, vaa soksi na viatu vya kufunika ili miguu iendelee kuwa na unyevu, wakati wa usiku pia fanya hivyo huku ukilala miguu imevalishwa soksi baada ya kuipaka mafuta.
Ambatanisha vitu vifuatavyo katika mlo wako, vyakula venye madini ya calcium, zinc na iron. ( Maziwa, mboga za majani, mafuta ya mimea, nyama, maharage pamoja na samaki wa maji baridi).
Kuepuka kusimama kwa muda mrefu pamoja na kutoiweka miguu katika maji kwa kipindi kirefu. Kama unafanya zoezi la ufuaji, jitahidi kuilinda miguu yako isiwe katika sabuni kwani sabuni nyingi za kufulia huvunjavunja mafuta yaliyo katika ngozi na kuiacha ikiwa kavu sana na kuifanya ipasuke.
Jitahidi walau mara moja kwa wiki, kuiweka miguu yako katika maji ya vuguvugu, hii husaidia kuongeza mzunguko wa damu katika miguu na hivyo kuendelea kuimarisha afya ya ngozi yako.
Tunaamini kabisa kwamba siyo siku zote huwa zinafanana. Mara nyingine siku huanza vema na kuendelea kwa furaha amani na mafanikio hadi mwisho wa siku hiyo.