Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Yegomasika wea a yuuu??
36ed04111fb40c791f67a0bf008eb641.jpg
 
Haya mambo ndugu yangu ni magumu. Hawa wanakuwa ni watu mnaoishi nao. Kaka, baba, wana na hata dada. Mchana mnajichanganya nao na muda ukifika hao wanawageuka na kwenda kufanya yao. Ndilo tatizo pia walilokumbana nalo Wamarekani huko Afghanistan. Hujui adui yako ni nani na makamanda wengi wanakiri kuwa vita vya aina hii ndivyo vigumu zaidi kupigana, unless uwe katili uue na raia wasiohusika.

Na wakati mwingine hata kama adui anajulikana, inakuwa vigumu kumtokomeza kutokana na weledi wake wa mazingira aliyomo na umahiri wake wa kujishabihisha nayo. Ndiyo maana mpaka leo Joseph Kony bado yupo na jeshi lake. Kwa nini jeshi la Uganda lisiende tu na kumwangamiza mara moja? Ndiyo maana Dos Antos alihangaika na Savimbi kwa miongo kadhaa. Ndiyo maana kule Colombia waasi wa FARK wamejichimbia msituni huko wanalima coca wanauza na kuendelea kupambana kwa miaka pamoja na madege ya Kimarekani yenye teknolojia ya kila aina kuwasaka mchana na usiku. Afghanistan mataliban wamejichimbia mapangoni huko milimani na Wamarekani hawathubutu kutia mguu huko kwa sababu wanajua kuwa wataangamia. Sana sana wanaishia tu kudondosha mibomu yao ya kilo 500 na kukimbia....

Kwa kifupi, mtu akiamua kujitoa mhanga kupambana na kupigania kile anachokiamini, siyo rahisi kumtoa katika mhimili wake aliojiwekea hata uwe na silaha na jeshi lenye nguvu namna gani. Ndiyo maana migogoro mingi ya aina hii huishia kutatuliwa kwa majadiliano. Na kibaya zaidi, unakuta migogoro hii wakati mwingine inachochewa na hao hao wa upande mwingine kwa sababu zao binafsi, kisiasa na vinginevyo. Ni shida mkuu....
Kama hivyo ndivyo serikali ya Nigeria iache kiburi, iingie kwenye majadiliano ya kusaka AMANI ya taifa lake. Kuongea na watu ambao umewashindwa kivita siyo kosa. kubwa hapa ni kuwafanya wazee, watoto na akina mama wa Nigeria wanaishi kwa furaha nchini mwao
 
Back
Top Bottom