Pimbi ni jamii ya wanyama wenye maumbile madogo na vimo vifupi sana ambao wanapatikana maeneo mbalimbali hasa barani Afrika. Ni jamii moja tu ya pimbi ambayo inapatikana nje ya bara la Afrika na maeneo ya ghuba za Arabuni kutokea nchi ya Lebanon hadi maeneo ya Saudi Arabia. Wanyama hawa kutokana na maumbile yao madogo huwa ni vigumu sana kuwaona na bila kuwa makini unaweza zunguka hifadhini hata mwezi mzima bila kuwaona kwani huwa wana tabia ya kujificha sana kwenye mazingira wanayoishi. Hivyo unapokuwa unatalii katika hifadhi za wanyamapori unapaswa kuwa makini zaidi katika uchunguzi hasa maeneo yenye miamba.