Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Rolls royce phantom v lina sifa za kipekee kwa wakati huo likionekana ndiyo gari la kisasa zaidi kwani lilikuwa na sehemu mbili za kuwekea bendera. Pia rais wa awamu ya pili wa tanzania naye alitumia gari hilo na rais wa awamu ya tatu naye alitumia gari hilo na mnamo mwaka 2006 aliamua kulipeleka katika makumbusho ya taifa na kuwa sehemu ya historia..
 
2:MERCEDZ BENZ 230.6
-Gari hili lilijulikana kama gari la jumuiya kwani hayati mwalimu julius kambarage nyerere alilitumia kwa shughuli za jumuiya ya afrika mashariki iliyoundwa mwaka 1967 na nchi za Tanzania, Uganda na Kenya.
 
IMG-20180311-WA0024.jpg
 
Sifa moja ya gari hili lilikuwa na uwezo wa kubeba watu wengi zaidi, mercedz benz 230.6 lilikuwa na namba za kipekee ambazo ni RE-1( ikimaanisha royal excellency 1) mnamo mwaka 2002 gari hili lilipelekwa makumbusho ya taifa.
 
3:USTIN MORRIS A-40
-Gari hili lilitengenezwa nchini uingereza kati ya mwaka 1940-1950 ni gari la kwanza kutumiwa na rais wa kwanza wa tanzania mwalimu julius kambarage nyerere. Alilitumia gari hili katika shughuli mbalimbali hasa kuendeleza chama cha TANU likiendeshwa na dereva wake maarufu kwa jina la SAID TANU. Na hapo mwalimu alikabidhi gari hilo kwa vijana wa tanu katika kazi za chama , na baadae kuja kupelekwa kwenye makumbusho ya taifa na kuwa sehemu ya historia ya nchi.
 
4:MERCEDSS BENZ E- 300
-Gari hili lilitengenezwa nchini ujerumani na kununuliwa na serikali ya tanzania mnamo mwaka 1996 ambapo baba wa taifa alilitumia katika shughuli zake binafsi na za kitaifa. merceds benz e-300 litaendelea kukumbukwa kwani ndyo gari ya mwisho kutumiwa na mwalimu julius kambarage nyerere enzi za uhai wake na kwa mara ya mwisho alilitumia mnamo agosti 31,1999 akienda kupata matibabu huko nchini uingereza.
 
Hata hivyo hakurudi kulitumia gari hilo tena kwani alifariki mnamo oktoba 14,1999 katika hospitali ya mtakatifu thomas nchini uingereza,
mnamo mwaka 2004 gari lake lilitolewa na mkewe mama maria nyerere kwa ajili ya kuhifadhiwa katika makumbusho ya taifa.
 
5:ROLLS ROYCE
-Gari aina ya rolls royce lilitengenezwa mnamo mwaka 1938 na kuletwa na gavana wa wakati huo HAROLD MAC MICHAEL katika utawala wa wakoloni wa waingereza na likatumiwa na gavana wa mwisho kuitawala tanganyika SIR. RICHARD TURNBULL.
 
gari hili lilitumika hadi mwaka 1962 baadaye rais wa kwanza wa tanzania aliamuru gari hilo kuhamishwa kutoka ikulu mpaka katika makumbusho ya taifa. na kuwa sehemu ya historia ya taifa la tanzania.
haya ndiyo magari aliyotumia hayati MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE katika enzi za uhai wake hapa nchini na duniani.
 
Ndiyo natoka mkuu. Hapa niko "mtakatifu" balaa. Hata mamisambwanda nayakaushia tu sigeuzi shingo wala lile jicho la kuibia ibia. Niko fokasidi balaa. Ngoja nione hii hali itadumu mpaka lini [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Hata haitafika mid night [emoji23][emoji23][emoji23]tena mid night ni mbali nahisi hata jioni haifiki[emoji125] [emoji125]
 
Back
Top Bottom