Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

B. Njia ya upasuaji.
Njia kadhaa za upasuaji zipo kwa kuondoa mawe kwenye figo baada ya kushindwa kutoka kwa matibabu. Njia hizi hazishindani bali hukamilishana. Madaktari bingwa huamua ipi ni njia bora. Baadhi ya njia zinazotumika sana ni pamoja na: (i) Njia ya kutovunjavunja mawe kwa njia ya mashine. (ii) Njia ya kuyatoa mawe kwa kutengeneza njia hadi kwenye figo kupitia mgongoni. (iii) Njia ya kutoa jiwe/mawe kupitia kwenye njia ya mkojo na. (iv) Upasuaji wa kawaida.
 
Ni mgonjwa yupi huhitaji upasuaji?
Wengi huweza kutolewa mawe bila upasuaji lakini kuna wale lazima wapitie upasuaji kwa mfano:

Jiwe likikataa kutoka baada ya muda wa kutosha /mwingi na kusababisha maumivu makali.
Jiwe ni kubwa sana na linashindikana kutoka/kuteremka lenyewe.
Jiwe linapozuia mkojo na kwa hiyo kudhuru figo.
Jiwe linaposababisha maambukizo ya njia ya mkojo au kutokwa na
damu.
 
Ni mgonjwa yupi huhitaji upasuaji?
Wengi huweza kutolewa mawe bila upasuaji lakini kuna wale lazima wapitie upasuaji kwa mfano:

Jiwe likikataa kutoka baada ya muda wa kutosha /mwingi na kusababisha maumivu makali.
Jiwe ni kubwa sana na linashindikana kutoka/kuteremka lenyewe.
Jiwe linapozuia mkojo na kwa hiyo kudhuru figo.
Jiwe linaposababisha maambukizo ya njia ya mkojo au kutokwa na
damu.
 
nzuri kwa kutoa mawe yenye ukubwa usiozidi sentimita moja na nusu,au mawe yaliyo katika njia ya mkojo katikati ya kibofu na figo (ureta).

Mawe huvunjwa kwa mawimbi yanayotoka kwenye mashine na huyavunja katika vipande vidogo vidogo ili yaweze kutoka kwenye mkojo kirahisi.Mgonjwa hutakiwa kunywa maji mengi wakati mwingine baada ya tiba hii. Tyubu ya plastiki nyororo huwekwa ndani ya njia ya mkojo ili kuzuia kuziba kwa njia hiyo.
 
3. Kuzuia mawe ya asidi ya yurik
Epuka vileo vyote.
Jiepushe na nyama ya maini,figo,ubongo,pia samaki,nyama ya nguruwe,kuku,ng‘ombe,na hata mayai.
Jiepushe pia na maharagwe, spinechi, dhania, koliflawa na mkate mfamu.
Jiepushe na vyakula vyenye mafuta kama aiskrimu na vilivyokaangwa.
Tumia dawa kama zile za kuzuia aside ya yurik.
Zuia uzito usizidi.
Basically hakuna kula cho chote...
 
Kwa ujumla njia hii huwa salama na matatizo yake ni kama damu kwenye mkojo,maambukizi,mawe kubaki na hivyo kuhitaji marudio ya matibabu haya,kudhuru figo na shinikizo la damu.Uzuri wake ni huwa ni njia salama ambayo haihitaji kulazwa hospitalini,dawa ya nusukaputi wala kukatwa.Uchungu si mwingi na inafaa kwa umri wowote ule.
 
Njia hii haifai kwa mawe makubwa na kwa watu wanene.Pia si nzuri kwa wajawazito na watu wenye maambukizo makali, shinikizo la damu au matatizo ya kutokwa na damu.Baada ya kutolewa mawe,lazima mgonjwa aangaliwe na daktari mara kwa mara na pia azingatie njia za kuzuia mawe kutokea tena.
 
Back
Top Bottom