Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

2. Njia ya kupitia mgongoni
Njia hii ni bora kwa mawe makubwa namakubwa kadri yenye Ukubwa zaidi ya sentimita moja na nusu.Hutumiwa mara nyingi wakati njia nyingine zimeshindwa.
 
3DADD651-E048-4820-BD80-647A24081E2C.jpeg
 
Katika njia hii mgonjwa hudugwa sindano ya nusukaputi na daktari hukata shimo dogo mgongoni na kutengeneza njia kutoka kwenye ngozi hadi kwenye figo.Hutumia mashine inayoonyesha viungo vya ndani pia.Huku akitumia mashine nyingine, daktari hulipata na kulitoa jiwe.Iwapo ni kubwa,jiwe huvunjavunja kwa mawimbi yenye nguvu na kisha vipande hivyo hutolewa
 
Kwa ujumla,njia hii huwa salama ingawaje kuna hatari na matatizo yanayoweza kutokea, jambo ambalo ni la kawaida kwa upasuaji wowote ufanywapo.Matatizo haya yanaweza kuwa kutokwa na damu,maambukizo,kujeruhi viungo vilivyo karibu au mkojo kumwagika.Uzuri wake ni kuwa ni sehemu ndogo tu hukatwa(kama sentimita moja).Njia hii ni nzuri kwa mawe yoyote.Mgonjwa huwa hospitalini kwa muda mfupi tu na hupona haraka.
 
3. Kupitia njia ya mkojo
Njia hii ni bora ya kutoa mawe yaliyo katikati na upande wa chini wa njia ya mkojo.Mgonjwa hudugwa sindano ya nusukaputi kisha tyubu yenye kamera huingizwa hadi kwenye kibofu cha mkojo na kuingia kwenye yureta.Jiwe huweza kuonekana na hutolewa zima zima au huvunjwavunjwa kutegemea na ukubwa wake.Kama jiwe ni dogo ,hushikwa na kutolewa kwa mashine hii,kama ni kubwa, huvunjwavunjwa na hivyo basi vipande hivi vidogovidogo hutoka na mkojo.Mgonjwa hurudi nyumbani siku hiyo hiyo na huweza kuendelea na shughuli za kawaida baada ya siku mbili au tatu.
 
Faida za njia hii ni kuwa hata mawe magumu yanaweza kuvunjwa na haihitaji kukatwa/kupasuliwa (Incision).Ni salama kwa mama wajawazito,watu wanene na wenye matatizo ya kutokwa na damu.Matat izo yanayoweza kutokea ni damu kwenye mkojo,maambukizi,kujeruhiwa/kutoboa ureta na kuwa kovu baada ya kupona ambalo hupunguza upana wa yureta.
 
Back
Top Bottom