Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

29094187_360234074478191_3650343054772011008_n.jpg
 
MWANAMITINDO ambaye ni kada wa CCM, Jokate Mwegelo ambae pia ni Kaimu Katibu Hamasa wa Jumuiya ya Vijana CCM, ameibuka na kudai anatarajia kuolewa ‘kuwa mke wa mtu siku za hivi karibuni’ licha ya kumficha mwanaume ambaye atamuoa.
Jokate ametoa kauli hiyo mchana wa leo kupitia ukurasa wake wa kijamii akiwa wahabarisha wadau wake wakae mkao wa kula kusherehekea tukio hilo ambalo amelipanga kulifanya katika siku za usoni.
 
“March Quen, karibu nitakuwa mke wa mtu fulani na mama watoto wake. ‘God is great and faithful, grown but forever a baby girl’. Ni kwa neema tu na rehema zake Mungu. Thank you loves for dragging me out to take these”, amesema Jokate.
Jokate Mwegelo ameweza kuweka uwazi wa maisha yake ndani ya siku aliyoweza kuletwa duniani ‘kuzaliwa’ miaka kadhaa iliyopita tarehe na mwezi kama wa leo.
 
MWANAMUME mmoja aliyejulikana kwa jina Bernard Shumba mkazi wa Singida anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani humo kwa kumuua mke wake miaka minane iliyopita kisha kuuficha mwili wa marehemu kwenye mbuyu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Deborah Magiligimba, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema mtuhumiwa baada ya kukamatwa alikiri kutenda kosa hilo na kwenda kuonyesha mwili wa marehemu aliokuwa ameuhifadhi ndani ya mbuyu ambapo jeshi hilo kushirikiana na wananchi limefanikiwa kupata mabaki yake.
w4.jpg
 
Inadaiwa kuwa mnamo Julai 10, 2010 katika Kijiji cha Yulansoni Kata na Tarafa ya Kinyangiri Wilaya ya Mkalama mkoani Singida, Tabu Robert (28) ambaye kwa kabila ni Mnyiramba, mkulima wa Yulansoni, aliuawa na mume wake aitwae Bernard Shumba Siza (47), Mnyiramba na mkulima wa Yulansoni.
w2.jpg
 
Baada ya Mmuhumiwa kufanya tukio hilo aliuchukua mwili wa marehemu na kwenda kuuficha kwenye mti wa mbuyu ambao una tundu kubwa na kisha aliripoti polisi kituo kidogo cha Kinampanda Mkalama kuwa mke wake ametoroka na alianza kumtafuta hadi tarehe Machi 17, 2018 ambapo taarifa zilipopatikana kuwa alimuua.
w1.jpg
 
Baada ya mtuhumiwa kukamatwa na kuhojiwa alikiri kufanya kitendo hicho na kuonyesha sehemu alipouficha mwili huo Machi 18, mwaka huu majira ya saa 10:00 jioni.
Mkuu wa polisi kituo cha Mkalama na timu yake ya makachero walifika eneo la tukio na kufanikiwa kupata mabaki ya mifupa yakiwa ndani ya mti huo. Baadhi ya mifupa imechukuliwa kwa ajili ya kupelekwa kwa mkemia wa serikali na iliyobakia ndugu wamekabidhiwa kwa ajili ya mazishi.
 
Baada ya Mmuhumiwa kufanya tukio hilo aliuchukua mwili wa marehemu na kwenda kuuficha kwenye mti wa mbuyu ambao una tundu kubwa na kisha aliripoti polisi kituo kidogo cha Kinampanda Mkalama kuwa mke wake ametoroka na alianza kumtafuta hadi tarehe Machi 17, 2018 ambapo taarifa zilipopatikana kuwa alimuua.View attachment 721203
Dah!
 
Back
Top Bottom