Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

JIWEKEE NEMBO BORA
Wazungu huita jambo hili kwa jina la brand. Kwenye bidhaa au kazi zako jiwekee nembo ya kudumu ambayo itakuwa utambulisho wako. Ifike mahali kama mtu anahitaji huduma yako, ajue moja kwa moja wewe umejikita kwenye eneo gani.
 
Mfano, Rais wa Marekani wa sasa na mfanyabiashara mkubwa, Donald Trump anajua faida ya nembo. Jina lake linatumiwa na wafanyabiashara wengi mno duniani na wanamlipa pesa nyingi. Kuna wanaotengeneza tai na kuziandika jina lake, wengine wanatengeneza mvinyo (wine) na kuziita kwa jina lake na bidhaa zingine nyingi.
 
Na wewe ninakushauri ujiwekee nembo bora ya kudumu katika kazi zako. Mfano hapa nchini, ukitaja neno hadithi, asilimia tisini ya Watanzania watakutajia Shigongo, ingawa kuna wengine wa vizazi vya nyuma kama marehemu Ben Mtobwa na Elvis Musiba. Watu hawa walijitengenezea nembo kwenye eneo hilo, maisha ni kujitambua wewe ni nani na umekuja kufanya nini duniani, pambana kutimiza malengo ya wewe kuzaliwa.
 
TENGENEZA MTANDAO
Jitahidi sana kujitanua kwa kufahamiana na watu wengi kadiri uwezavyo. Mipango au kama ambavyo vijana wa kisasa huita michongo mingi iko kwa watu. Kadiri unavyofahamiana na watu wengi ndivyo unavyojiongezea fursa nyingi za kujipatia pesa kwa sababu wingi wa kufahamika kwako na biashara yako ni wingi na ongezeko la wateja na pesa!
 
NIDHAMU
Nidhamu imegawanyika katika makundi makuu matatu. Nidhamu kwa watu, muda na pesa. Mfanyabiashara yeyote kama hana nidhamu ni vigumu mno kupiga hatua zaidi. Ni lazima ujiwekee nidhamu kwa watu. Heshimu watu wote ingawa usipitilize na kuwa kama unawaabudu.
 
Mchukulie kila aliye mbele yako kama sababu ya wewe kufungua biashara yako. Ona kabisa kutoka moyoni mwako kwamba bila yeye usingeanzisha biashara kwa sababu umefungua biashara hiyo ili uhudumie watu, sasa kama watu hao huwaheshimu, unadhani wao watakuheshimu wewe na kujali biashara yako? Jibu unalo.
 
ONDOA KABISA MATUMIZI YASIYOKUWA YA LAZIMA
Hiki ni kipengele ambacho huwashinda watu wengi sana. Hivi karibuni nilipata nafasi ya kumsikiliza tajiri wa Kitanzania kijana zaidi, Mohamed Dewji ‘Mo’ juu ya namna ambavyo hutumia pesa zake. Hakika nilibaki mdomo wazi na nikajifunza kabisa kwamba kumbe matajiri hawana matumizi ya kufuja kama ilivyo kwa masikini ambao utapanyaji wao wa pesa ni mkubwa tofauti kabisa na vipato vyao.
 
Back
Top Bottom