Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

WAKATI mashabiki wa muziki wa dansi walimsubiria kwa muda mrefu, nguli wa muziki huo, Ngiama Makanda maarufu kama Werrason kutua jijini Dar kwa shoo ambayo ingefanyika juzi Ijumaa katika kiwanja cha Escape One jijini Dar es Salaam, hatimaye ametua jijini Dar es Salaam alfajiri ya kuamkia leo Jumapili.
 
Nguli huyo kutoka Jamahuri ya Kidemokrasia ya Congo ametua na Ndege ya Shirika la Kenya (Kenya Airways) alfajiri ya Jumapili akitokea Kinshansa na yuko tayari kwa kukonga nyoyo za mashabiki wake.
 
Akizungumza na MCL Digital mmoja wa waratibu wa shoo hiyo, Yale Ngossi amesema walichokuwa wanasubiri kufika kwa Werrason na baada ya hapo mipango ya shoo inapangwa upya hivyo mashabiki wataambiwa tarehe ya kufanyika onyesho hilo.
 
Kwanza tunashukuru kwa ujio wake Werrason na pia baadaye tutakaa tupange shoo ifanyike lini maana tulikuwa tunasubiri afike kwanza ndio tupange tarehe. Hapa ni tunaanza upya, ila kwa wale wenye tiketi walizokata mara ya kwanza shoo ilivyoahirishwa, watazitumia hizo, ila chondechonde wasije jitokeza watu na tiketi feki na kusema ndizo walizokata mara ya kwanza, yaani tumejipanga kwa hilo,” alisema Yake Ngossi.
 
Werrason amekuja na wanamuziki wake 10 na wengine 14 wataingia leo, ambao watafikisha jumla ya wanamuziki ishirini na nne.
 
Siri imefichuka kocha wa Manchester City, Pep Guardiola alitaka kumsajili kiungo wa Manchester United, Paul Pogba.

Guardiola alitaka kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa katika usajili wa dirisha dogo Januari, mwaka huu.
 
Raiola alikiri kuzungumza na Guardiola, lakini walijikita katika kuizungumzia Man City siyo mteja wake.

“Sikuwahi kuzungumza na Guardiola kuhusu usajili wa Pogba, ni kweli tulizungumza, lakini tulizungumzia Man City nilimsifu kwa mafanikio,” alisema wakala huyo maarufu
 
Uhusiano baina ya Pogna na bosi wake Jose Mourinho umekuwa wa kuasua na wakala huyo ametishia kumuondoa nyota huyo Man United.

Mchezaji huyo amekuwa akisugua benchi tangu kuanza msimu huu licha ya kumnunua kwa bei mbaya kutoka Juventus ‘Kibibi Kizee’ cha Turin.
 
Back
Top Bottom