Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Inakuwa na lile swali maarufu la cole hahahahah

20180404_134447.jpg
 
Uhusiano baina ya Pogna na bosi wake Jose Mourinho umekuwa wa kuasua na wakala huyo ametishia kumuondoa nyota huyo Man United.

Mchezaji huyo amekuwa akisugua benchi tangu kuanza msimu huu licha ya kumnunua kwa bei mbaya kutoka Juventus ‘Kibibi Kizee’ cha Turin.
 
SUPASTAA wa Nice, Mario Balotelli ameibuka na madai kwamba rangi yake ya ngozi ndiyo tatizo kubwa linalomfanya asichaguliwe kuichezea timu ya taifa ya Italia kwa muda mrefu sasa.

Fowadi huyo aliwahi kuzichezea Manchester City na Liverpool huko England alisema angekuwa na matatizo machache sana kama ngozi yake ingekuwa nyeupe akiwa na maana ya kwamba kama angekuwa mzungu. Hata hivyo, Balotelli akajitetea kwamba hadhani kama nchi yake ya Italia ni ya kibaguzi
 
Balotelli yupo kwenye kiwango bora kabisa huko Nice kwa sasa, akiwa amefunga mabao 22 katika michuano yote aliyocheza msimu huu, lakini hajachaguliwa kuichezea Azzurri kwa muda mrefu na mara ya mwisho ilikuwa kwenye fainali za Kombe la Dunia 2014 zilizofanyika Brazil.

Tangu wakati huo hajachaguliwa tena kwenye timu ya taifa na Balotelli anasema hilo haliwezi kuwashtua mashabiki kwa sababu hawamhesabii kuwa ni Mtaliano, licha ya kwamba alizaliwa na kukulia katika nchi hiyo.
 
Balotelli alisema: “Kuna baadhi ya viwanja mashabiki wamekuwa wakishangilia “hakuna Mtaliano mweusi” wakielekeza hilo kwangu, lakini nataka kuwaambia Wataliano weusi wapo. Unajua nini, hata kama mimi ni Mtaliano, nilizaliwa na kukulia Italia, lakini sheria zao zilinithibitisha kuwa ni Mtaliano baada ya kufikisha miaka 18. Sheria hiyo ina kasoro kubwa na ndio watu weusi wanaonekana kuwa ni rangi ya ovyo.”
 
UNAAMBIWA hivi, Kevin De Bruyne ameweka upinzani kali na kukubali kwamba Mohamed Salah ni mkali kwa msimu huu baada ya kumpigia kura ya kumtaka ashinde tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa England. Kiungo huyo wa Manchester City, De Bruyne anachuana jino kwa jino na fowadi huyo wa Liverpool, Mo Salah kutokana na viwango vyao bora wanavyovionyesha kwenye mikikimikiki ya Ligi Kuu England msimu huu.
 
Back
Top Bottom