Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mara nyingi kina mama huwa na msemo, “Ninachokitaka maishani ni kumuona mwanangu ana furaha.”

Hicho ndicho alichokifanya Dafroza Limandola aliyeamua kutoa figo yake moja na kupandikizwa kwa mtoto wa dada yake, Asha Athuman (28).
 
Huyu ni mwanangu. Ni mtoto wa dada yangu, mama yake alifariki miaka mingi, najisikia furaha kuokoa maisha yake, sioni tatizo lolote,” alisema Dafroza muda mfupi baada ya Asha na mwenzake waliokuwa wamepandikizwa figo kuruhusiwa kutoka hospitalini jana.

“Sio figo moja tu, nilikuwa tayari kutoa hata zote mbili ili mwanangu aendelee na maisha yake. Kuna maana gani kuwa na figo zote wakati mwanao anakufa?” alisema Dafroza kwa msisitizo.
 
Asha ni miongoni mwa wagonjwa wanne waliopandikizwa figo Aprili 18 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) na jana, yeye na Suzana Thomas (22) waliruhusiwa kutoka hospitali baada ya afya zao kuimarika huku wengine wawili wakiendelea na matibabu.

Dafroza alisema amefurahi mno kuona binti yake akipata matibabu baada ya kuugua kwa muda mrefu
 
Binti amwaga machozi, ashukuru

Wakati Dafroza akisema hayo, Asha alikuwa akitoa machozi ya furaha na alimshukuru mama yake mdogo kwa kuokoa maisha yake.

“Sikutegemea kama mama yangu mdogo angeweza kuhatarisha maisha yake kwa ajili yangu,” alisema Asha.
 
Asha ambaye ni mtumishi wa Manispaa ya Ubungo, ni miongoni mwa wagonjwa wa tano ambao wameshafanyiwa upandikizaji huo wa figo Muhimbili. Wa kwanza ni Prisca Mwingira aliyepandikizwa Novemba mwaka jana.

Suzana aliwashukuru wauguzi na madaktari wa Muhimbili kwa huduma bora.“Namshukuru Mungu, sikutegemea kama ningepona. Nawashukuru madaktari, wauguzi na Serikali kwa kuratibu matibabu yetu na leo hii tunarudi kwenye maisha ya kawaida,” alisema.
 
Daktari azungumzia mikakati

Mkuu wa Kitengo cha Figo cha MNH, Dk Jackline Shoo alisema kuwa upandikizaji huo ni hatua kubwa na imedhihirisha kuwa madaktari wa Tanzania wanaweza.

Alisema wagonjwa wote waliopandikizwa wanaendelea vizuri, lakini wamewaruhusu wawili huku wakiendelea kuwafuatilia waliosalia.
 
Back
Top Bottom