Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kuna huyu mwingine pyaar ndio balaa kabisa jana amenikomalia hapa, akidai Eksipiriensi anayo yakutosha ya kunilea
Mpaka nikatafuta video ya Jack pemba nione anavyolelewa ni hatari bro
Woyooo mambo ni motroooo[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Daktari azungumzia mikakati

Mkuu wa Kitengo cha Figo cha MNH, Dk Jackline Shoo alisema kuwa upandikizaji huo ni hatua kubwa na imedhihirisha kuwa madaktari wa Tanzania wanaweza.

Alisema wagonjwa wote waliopandikizwa wanaendelea vizuri, lakini wamewaruhusu wawili huku wakiendelea kuwafuatilia waliosalia.
 
Alisema ni matamanio yake kuona kitengo hicho kinakuwa na uwezo wa kuwahudumia watu wengi zaidi kutoka ndani na nje ya nchi.

“Tunashukuru Serikali kwa kutuwezesha, tunaomba iendelee kutuona ili wigo wa huduma zetu upanuke, tuwahudumie hata watu kutoka nje ya nchi,” alisema.
 
Niwasihi Watanzania wenye matatizo haya wasisite kwenda hospitali, madaktari wapo na huduma hizi zinapatikana hapahapa kwetu kwa gharama nafuu.”

Maisha baada ya kutoa figo

Akizungumzia hali ya kiafya kwa mtu aliyetoa figo na aliyewekewa mpya, Dk Shoo alisema anatakiwa kuangalia hali yake kama aliyefanyiwa upasuaji.
 
Kwa aliyetoa alisema, “Baada ya miezi mitatu anaweza kuanza kufanya kazi nyepesi ambazo hazitamchosha kwa kuwa mwili wake una figo moja.”

Kwa aliyewekewa figo, alisema anatakiwa kujiweka mbali na mikusanyiko ya watu kutokana na kuwapo uwezekano wa kupata maradhi kwa haraka kwa kuwa dawa anazotumia hushusha kinga ya mwili.
 
Kuhusu chakula, Dk Shoo alisema anaweza kula vyakula vyote isipokuwa kama alikuwa na ugonjwa mwingine ambao una masharti ya vyakula.

Kwa aliyetoa figo, alisema baada ya mshono kupona kabisa anaweza kjuendelea na shughuli zake kama kawaida ikiwamo tendo la ndoa. Hata hivyo, alisema kama ni mwanamke atatakiwa kujichunga kupata ujauzito kwa kipindi cha miezi sita hadi mwaka mmoja.
 
Kwa aliyepandikizwa, alisema anaweza kuendelea na shughuli zake kama kawaida baada ya miezi sita.

Hata hivyo, alisema mtu huyo pia anaweza kushiriki tendo la ndoa baada ya kidonda kupona lakini akaonya kwamba mwanamke haruhusiwi kubeba ujauzito kwa kipindi cha miaka miwili. Alisema katika kipindi hicho, mama huyo atakuwa akitumia dawa ambazo zinashusha kinga na ambazo si salama kwa mtoto. “Atakapokuwa tayari kubeba mimba, atatakiwa atoe taarifa ili abadilishiwe dawa.”

Mengine ni kuacha pombe na kuvuta sigara.
 
Jengo jipya Muhimbili

Akizungumzia mkakati wa baadaye wa utoaji wa huduma hiyo, Mkurugenzi wa Mawasiliano Muhimbili, Aminiel Eligaesha alisema hospitali hiyo ipo mbioni kujenga jengo la ghorofa saba ambalo ndani yake kutakuwa na ghorofa moja itakayokuwa maalumu kwa ajili ya wagonjwa wanaotakiwa kupandikizwa figo.
 
Eligaesha alisema uwepo wa ghorofa hilo utawezesha wastani wa wagonjwa 200 hadi 250 kupandikizwa figo kwa mwaka. Alisema ujenzi wa jengo hilo utaanza kati ya Mei na Juni ikiwa ni sehemu ya mipango ya muda mrefu ya kukabiliana na tatizo la ongezeko kubwa la wagonjwa.

Mpango wa Wizara ya Afya ni kupandikiza figo kwa wagonjwa 60 kila mwaka.
 
Back
Top Bottom