Kwa aliyepandikizwa, alisema anaweza kuendelea na shughuli zake kama kawaida baada ya miezi sita.
Hata hivyo, alisema mtu huyo pia anaweza kushiriki tendo la ndoa baada ya kidonda kupona lakini akaonya kwamba mwanamke haruhusiwi kubeba ujauzito kwa kipindi cha miaka miwili. Alisema katika kipindi hicho, mama huyo atakuwa akitumia dawa ambazo zinashusha kinga na ambazo si salama kwa mtoto. “Atakapokuwa tayari kubeba mimba, atatakiwa atoe taarifa ili abadilishiwe dawa.”
Mengine ni kuacha pombe na kuvuta sigara.