(b) Kupwa na Kujaa kwa Bahari (Ocean Tides) or ( Lunar Tides)
Kupwa na kujaa kwa maji hutokea baharini na pia kwenye maziwa makubwa, mwezi na dunia siku zote huvutana, mwezi huwa unajaribu kuvuta chochote kilichopo duniani ili ikisogeze karibu wakati huo huo dunia nayo huvivuta vitu vyake viendelee kubaki katika dunia. (The Earth’s gravity against The moon's Gravity)
Maji ni kitu kisichotulia sehemu moja na hubadirika umbo kirahisi sana, hivyo mvutano huu huyafanya maji kuelekea kule mwezi ulipo na hapa ndio kitendo cha kupwa na kujaa kwa maji pamoja na mawimbi kutokea baharini.
Kwa wenyeji wa pwani nadhani hali hii ni ya kawaida kwao, kwani kuna wakati fulani ukienda baharini unakuta maji hayapo kipindi cha mchana na mida ya jioni maji hayo hurejea tena