Kipindi cha uhuru na ugawaji wa Uhindi
Ndani ya Uhindi wenyewe fitina ilianza juu ya nafasi ya Waislamu katika taifa jipya, huku sehemu kubwa ya Waislamu wakidai kugawiwa kwa koloni katika nchi mbili.
Mapigano yalianza na watu maelfu waliuawa. Mnamo Agosti 1947 nchi mbili za Uhindi naPakistan zilianzishwa, na Oktoba 1947 vitavikafuata kati ya nchi zote mbili juu ya jimbo la Kashmir. Vita vikaongeza uadui, na watu mamilioni walifukuzwa yaani Wahindu kutoka Pakistan na Waislamu kutoka Uhindi.
Gandhi alijitahidi kupatanisha viongozi wa pande zote akafunga chakula akitangaza alikuwa tayari kufunga hadi kifo wasipopatana. Heshima kwa Gandhi ilisababisha viongozi wa pande mbalimbali katika Uhindi kukutana na kutafuta njia za kumaliza uhasama.