Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

kuiba kunahitaji nyenzo. sio kila mtu anaweza...
Hicho ni kisingizio. Siku hizi unaweza kuwa Moscow lakini ukaiba kura za Florida au Mwanza. Wakiwekeza hizo billions za ruzuku, inawezekana kabisa jirani [emoji1549]‍♂️[emoji1549]‍♂️[emoji1549]‍♂️[emoji1549]‍♂️
 
KIUNGO Blaise Matuidi amewaambia wale wanaomtaka Cristiano Ronaldo afunge mabao watulie tu, mabao yatakuja kwani suala la kutupia wavuni lipo kwenye damu ya staa huyo wa Ureno.

Ronaldo hadi sasa ameshindwa kutikisa nyavu huko kwenye Serie A, akicheza mechi mbili tangu alipotua Juventus akitokea Real Madrid kwa ada ya uhamisho ya Pauni 99 milioni.

Mshindi huyo mara tano wa Ballon d’Or amefunga mabao 450 katika mechi 438 alizocheza kwa miaka yake tisa huko Real Madrid, lakini mambo yamekuwa magumu tangu atue Juventus, mechi mbili kwenye Serie A na hakuna bao alilofunga.
 
Lakini Matuidi alisema hana wasiwasi juu ya jambo hilo kwa sababu anamini katika uwezo wa mshambuliaji huyo linapokuja suala la kutupia mipira kwenye nyavu.

“Ni mchezaji bora duniani. Kwa upande wetu anakuja kutupa kitu tofauti, nimefurahi sana kwa kucheza naye timu moja,” alisema Matuidi.

“Tunafahamu wazi atakapofunga mabao yake yatatusaidia kushinda mechi nyingi zaidi.

“Tutakachofanya ni kumsaidia kufunga kwa sababu jambo hilo lipo kwenye damu yake.”
 
SUPASTAA wa Bongo fleva, Ommy Dimpoz's hali yake inaendelea kuimalika tofauti na mwanzo alipokuwa katika matatibu nchini Afrika Kusini.

Dimpoz's alisema alianza kufanyiwa vipimo vya afya yake nchini Kenya kwa kumkata kinyama cha shingo ili kubaini kama kweli ana kansa kama ilivyokuwa imedaiwa jijini Dar es Salaam, ambako alipima aliambiwa ana ugonjwa huo.
 
Nilipima hospital kubwa jijini Dar es Salaam, waliniambia nina kansa, lakini baada ya kupima Kenya ndipo nikaambiwa nililishwa sumu, nashukuru Mungu kwa maombi ya ndugu zangu, Watanzania na wasio Watanzania maombi yao yamenifanya nuru yangu irudi.

"Kikuweli kwa sasa naendelea vizuri nawaomba Watanzania waendelee kunikumbuka katika maombi yao nami nirejee katika majukumu nikiwa imara kiafya,” alisema Dimpoz.
 
Kamati ya Miss Tanzania imeweka wazi taji atakalovaa Miss Tanzania mwaka huu linathamani ya Sh6 milioni.

Mkurugenzi wa kampuni ya Look inayoendesha mashindano hayo Basila Mwanukuzi ameonyesha taji hilo litakalovaliwa na mshindi atakayepatikana Septemba 8.

Amesema sanjari na taji hilo mrembo atakayeibuka kidedea katika shindano hilo atapewa zawadi ya gari.

Mwanukuzi ameeleza kuwa kamati yake imeendelea kusimamia na kuhakikisha mrembo anapata zawadi bora na yenye viwango.
 
Amesema kulingana na maandalizi ya kamati hiyo mshindi atapewa gari zuri ambalo hata hivyo hakuweka wazi ni aina gani.

Kando na hilo alielezea utaratibu wa kupata tiketi ambazo mwaka huu zitauzwa kwa mfumo wa kielektroniki.

Meneja Masoko wa kampuni ya Otapp inayohusikan na uuzaji wa tiketi hizo Joachim Ferdinand amesema tayari tiketi timeshaanza kuuzwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…