Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mbunge wa Mtama Nape Nnauye ameandika katika ukurasa wake wa Twitter asubuhi ya leo August 31, 2018 “Barabara inapokua na shida, usikate tamaa na kuacha safari. Badili viatu na kusonga mbele!”

Alichoandika Nape wengi hawajafahamu ana maanisha nini? ila aliambatanisha na picha yenye maneno ya kizungu ambayo yeye aliyatafsiri katika caption.






Sent using Jamii Forums mobile app
 
MBUZI WANAVUTIWA NA BINADAMU WANAOTABASAMU.

Utafiti wa muonekano wa furaha wa mbuzi umefanyika Uingereza
Wanasayansi wamebaini kwamba mbuzi wanavutiwa na binadamu wanaotabasamu.
Utafiti huo umeelezea kwa kina namna ambavyo wanyama huwa wanatambua hisia za watu zaidi ya ilivyokuwa inafikiriwa awali.
Watafiti wamewaonesha mbuzi picha za mtu mmoja, moja iliyomuonyesha akiwa amekasirika na nyingine mtu huyo akiwana furaha.
Katika jarida la Open Science, watafiti wameeleza kwamba mbuzi hao walifanikiwa kuifuata picha ya mtu aliye na furaha.

Matokeo hayo yanadhihirisha kwamba uwezo wa wanyama kutafsiri hisia za binadamu sio mdogo ikilinganishwa na mbuzi ambao wameishi na kufugwa kama mbwa au farasi.
Badala yake inaonekana kuwa wanyama wanaofugwa kwa chakula. kama mbuzi pia wanaweza kutambua hisia usoni mwa binaadamu.
Watafiti wamebaini kwamba mbuzi wanapenda zaidi watu wanaotabasamu na kuzifuata picha za watu wenye furaha kabla ya kutambua picha za watu waliokasirika. Na pia walitumia pua zao zaidi kuzitambua vizuri picha za watu wanaotabasamu.
Lakini picha hizo za muonekano wa furaha ziliwapendeza zaidi zilipowekwa katika upande wa kulia.
Watafiti wanaamini huenda ni kwasababu mbuzi wanatumia upande wa kulia wa ubongo wao kutathmini matukio - jambo linalodhihirika kwa wanyama wengine.


Na picha hizo zilipowekwa katika mkono wa kushoto mbuzi hao hawakuonekana kuvutiwa nazo.
Inaweza ikawa upande wa kushoto wa ubongo ndio unatafakari hisia chanya au upande wa kulia wa ubongo ambao hauonesha sura ya hasira.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
WAVUVI WATUMIA KONDOMU KULINDA SIMU ZAO BAHARINI, Pwani, Kenya.

”Sisi hutumia mipira hii ya kondomu ili kulinda simu zetu kutoingia maji wakati tunapokuwa baharini tukiendelea na shughuli zetu za uvuvi”, alisema mmoja ya wavuvi hao.

Mvuvi huyo anasema kuwa wanapoingiza simu zao za mkononi katika mipira hiyo zinasalia kuwa salama na ni rahisi wao kuzungumza na wateja wao walio nchi kavu mbali na kuitisha msaada wakati wa hatari baharini.

Katika jamii za kihafidhina kama hii inayoishi pwani ya Kenya, mipira ya kondomu hushirikishwa na tendo la ngono.
Hivyo basi ununuzi ama hata ubebaji wake ni swala linalozungumzwa kwa siri kubwa kutokana na kazi yake.

Kwa wengi ni mwiko kuonekana na kinga hiyo , hatua inayoweza kuwashangaza wengi unapopatikana ukitembea na mipira ya kondomu ambayo hazijatumika mfukoni.

Kulingana na wavuvi hawa swala la wao kuelekea nyumbani wakiwa wamebeba paketi za mipira hiyo limekuwa la kawaida.


”Kwa sasa wake zetu wamezoea kwamba wakati mwingi sisi hutumia mipira hii kuzuia simu zetu za mkononi kuingia maji tunapokuwa baharini. Lakini kitambo ilikuwa vigumu kuelezea unapokamatwa na mipira hii ambayo mara nyingi husahaulika katika mifuko lakini tulikuwa tukiwaelezea kwa umakini hadi wanaelewa”. alisema mvuvi huyo.





Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji116][emoji116]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Serikali Kusimamia Vyakula vya Kwenye Harusi na Misibani Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) imewataka watoa huduma ya vyakula kwenye mikusanyiko ikiwemo kwenye misiba na harusini wajisajili na endapo wasipofanya hivyo watafungiwa.

Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Agnes Kijo, amesema, utoaji wa huduma ya chakula unapaswa kuzingatia sheria na kanuni bora za usafi ili kuhakikisha chakula kinachoandaliwa ni salama.

“Hatutaki tufikie hatua ya kufungiana biashara, kufikishana mahakamani bali tunahitaji watu wafate sheria kwa kujisajili ili watambulike na huduma wanazozitoa zizingatie usafi“, amesema Kijo.

Kijo amesema kuwa kwa sasa TFDA itakuwa na kazi ya kutoa elimu kwa watoa huduma hao ambapo watatoa muda maalum ili watu wajisajili baada ya hapo wataanza ukaguzi kwa kila halmashauri na itafikia hatua wataanza kusimamisha magari yaliyobeba vyakula ili kuyakagua.

Julai 13, akiwa ziarani jijini Mwanza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu alitoa agizo kwa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) na Wizara ya Afya, Kitengo cha Afya ya Mazingira, kuangalia ni Mamlaka ipi inajukumu la kutazama vyakula vinavyoliwa kwenye maharusi, ili kulinda afya za walaji.



[emoji39][emoji39][emoji39][emoji39]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…