Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

umri mkubwa...ni baraka kufika hapo
 
Ile siku haiwezi kusahaulika kabisa. Pyaar alilijibu alivyo ruhusu "kufukunyuliwa" kwa namna yoyote ile. Yaani ilikuwa raha sana [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Mambo na matani yetu ya humu ingekuwaga ni ukweli kuna watu wangekuwa na mimba sasa hivi. Eti "nifukunyue vyo vyote unavyotaka" lakini si ajabu ukimzukia laivu Gold Crest hutamsikia na JF haji. Shwaiini kabisa !!!
 
Barcelona wameripotiwa kwamba wamemweka kiporo kiungo wa Manchester United, Paul Pogba na kwamba watamfungia kazi ya kumsajili kwenye dirisha la majira ya kiangazi la mwakani.

Kwenye orodha ya wachezaji wengine inaowasaka Barcelona ambao imesema itawafanyia kazi mwakani ni staa wa PSG, Adrien Rabiot na kinda wa Ajax, Frenkie de Jong
 
Mabingwa hao wa La Liga walihusishwa na mpango wa kumsajili Pogba katika dirisha hili la majira ya kiangazi, lakini Man United wameripotiwa kugoma kumwaachia aondoke licha ya kupewa ofa ya Pauni 45 milioni pamoja na wachezaji Yerry Mina na Andre Gomes kwenye dili hilo ili tu Mfaransa huyo aende Nou Camp.
 
Kuhusu wachezaji wengine, Rabiot amekuwa mtu muhimu kwenye kikosi cha kocha Thomas Tuchel huko PSG, huku De Jong akifanya mambo makubwa akiwa na timu ya Ajax. Taarifa zinadai kwamba Barcelona itasajili wachezaji wawili kwenye orodha hiyo ili kuboresha safu yao ya kiungo kwenye dirisha la uhamisho wa majira ya kiangazi la mwakani.
 
Mshambuliaji wa kimataifa wa Ubelgiji, Nacer Chadli ameiacha West Bromwich Albion ya Ligi Kuu England na kujiunga na Monaco ya Ufaransa, kwa mkataba wa miaka mitatu.

Nyota huyo mwenye miaka 29, alisema anafurahia kurejea katika timu itakayomuwezesha kupata nafasi ya kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, ambayo ni ndoto ya kila mchezaji.
 
Alisema kilichomuondosha West Bromwich Albion ni timu hiyo kushuka daraja na akaahidi kufanya kila awezalo kuisaidia Monaco kupambana kusaka taji la Ufaransa ambalo kwa misimu saba mfululizo limetawaliwa na PSG.

"Nimefurahi sana kujiunga na AS Monaco, hii ni moja ya klabu kubwa nchini Ufaransa na yenye rekodi nzuri, kutoa mchango wangu hapa ni jambo kubwa kwangu binafsi,” alisema Chadli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…