Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

download%20(38).jpg
 
Kwanza, kulikuwa na kufikia kikomo cha sehemu ya pili ya urais wa Rais Ali Hassan Mwinyi ambaye alipokea uongozi kutoka kwa baba wa Taifa mwaka 1985. Hivyo, tayari kulikuwa na joto la Uchaguzi mwaka mmoja baadaye.

Pili, Uchaguzi huo wa 1995 ulikuwa ni uchaguzi wa kwanza katika taifa lililoungana ambapo vyama vingi vilikuwa vikishiriki. Kwa hiyo, mazingira ya kisiasa yalikuwa yasiyotabirika sana lakini yakiwa na mvuto wa pekee ndani ya CCM. Nje ya CCM vuguvugu lilikuwa halijapamba moto sana hadi pale Mrema alipojiengua na kuleta uhai mpya kabisa katika upinzani. Watanzania walikuwa wanaangalia kwa makini sana kile kilichokuwa kikiendelea ndani ya CCM kwani watu mbalimbali walikuwa wameshaanza kuonesha hamu na kiu ya kushika nafasi hiyo.

Tatu, matukio mawili yenye kuhusiana yalitishia moja kwa moja Muungano wa Tanzania kama ulivyo sasa yaani wenye muundo wa serikali mbili. Suala la Zanzibar kujiunga kwenye Jumuiya ya Nchi za Kiislamu (Organisation of Islamic Countries/Conferences -OIC) mwaka 1992 kulihusiana moja kwa moja na baadhi ya wabunge wa kutoka bara (waliojulikana kama G55) kutaka kudai kurudishwa kwa Serikali ya Tanganyika. Haya mawili (la OIC na hoja ya Tanganyika) bila ya shaka yalikuwa ndiyo sababu kubwa ya Mwalimu kuvunja ukimya na kuandika kijitabu hiki kuelezea kilichotokea miezi michache nyuma yake akijaribu kujenga hoja ya kuokoa mfumo wa muungano ambao yeye aliuasisi
 
Back
Top Bottom