uongozi wetu na hatima ya taifa letu
DIBAJI
Muundo wa kijitabu hiki ulivyokuwa mwanzoni umechanganya lugha ya kimashairi, mtiririko wa hoja, na kile ambacho naweza kusema ni mawazo huru ya Mwalimu juu ya masuala ambayo aliamini kuwa ni muhimu kwa taifa kujua. Kwa kila kipimo kijitabu hiki ni tafakari ya ndani ya Baba wa taifa kuhusu uongozi wetu katika kipindi kile cha historia na kwa namna fulani tunapata nafasi ya kuingia katika kichwa cha Nyerere na kuona mtiririko wa mawazo na hoja zake. Kwa namna ya pekee tunaweza kukiri kuwa Mwalimu Nyerere alikuwa na uwezo mkubwa wa kufanya mambo magumu yaeleweke kwa urahisi na masuala mazito yafahamike hata kwa mtu wa kawaida kabisa. Hivyo kijitabu hiki si kigumu kukielewa na wala si cha kifalsafa sana kama vitabu vyake vingine.
dah wavivu wa kusoma vitabu tunapata tabu sana, ni mwezi wa sita tokea nikipate kitabu hiki lakini cha ajabu ndio kwanza nakisoma tena kiuvivu uvivu.
huwa nashangaa sana ninapomuona mtu anajisifu kasoma vitabu 60 kwa mwaka tena vya kiingereza, huwa najiuliza amewezaje na ina maana hakai na kamusi akatafuta baadhi ya terminology?
kila paragraph nitakayoisoma itanibidi niuweke humu ndani ili wale wavivu wenzangu na wale wanaopenda kusoma maandishi angalau na wao wafute uchafu kwenye bongo zao..
mwisho wa siku sote tutakuwa tumefaidika.
au nakosea?