Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

FA018439-1F7F-4308-AE95-495DCD2E7034.jpeg
 
40522180_337454120131636_4454672431361797064_n.jpg
INAHUZUNISHA SANA Alizaliwa njiti (PREMATURE.😢) Wakati mke wangu alipokuwa anajifungua, nilikuwa nikifanya kazi. Daktari ambaye alikuwa akimhudumia mke wangu wakati wa ujauzito aliniita na kuniambia nifike hospitalini haraka iwezekanavyo. Nilipofika, nikamwona mtoto, nilikuwa ni kama nimefungwa mzigo wa kuni kwenye shingo, huku kichwa kikiniuma sana. Nilikaa chini na daktari aliniambia kuwa mke wangu ameondoka alipomwona mtoto ambaye hakuwa na msaada kwake, hivyo yeye alishuka kitandani na kuondoka licha ya hali yake aliyokuwanayo hakujali lolote, alisema kuwa huyo si mtoto wake na aliondoka kwa huzuni sana, hivyo ndivyo alivyoondoka. Daktari aliniuliza je! Ntafanya nini kwa huyu mtoto?, jibu langu halikuchukua hata sekunde moja, na bila kusita nilitumia nusu sekunde kumjibu Daktari kuwa "nitamtunza mtoto". Nilikuwa na maduka makubwa na yenye thamani. Lakini Niliuza maduka yote ili pesa nitakayopata imuhudumie na kumtunza mtoto huyu mchana na usiku. Akiba yangu yote, na pesa niliyopata kutokana na kuamua kuyauza maduka yangu, yote iliishia kwa mtoto wangu aliezaliwa kabla ya siku zake. Kiukweli Nilimpa moyo wangu wote, nikampa uvumilivu wangu wote, upendo wangu wote na akiba yangu kwani thamani yake huyu mtoto niliona ni zaidi kuliko kitu chochote. Nilimtunza mwenyewe bila msaada wa mtu isipokuwa daktari. Nilijitoa mwaka mmoja wa maisha yangu bila kufanya kazi bila kwenda mbali na yeye, tuliishi kwenye akiba yangu hadi leo na huyu mtoto wangu aliezaliwa kabla ya siku zake kutimia, mpaka sasa kufikia hatua ambayo anaonekana ni mvulana mzuri mwenye kuvutia tena mwenye afya njema. Mpaka kufikia hapo kuhusu hali ya mtoto aliyonayo ndio ikawa sababu ya mama yake kurudi na kutaka tuishi na kumlea mtoto wote ambapo ndio huyuhuyu mwenyewe aliemkimbia hospitalini kutokana na mwili wake na jinsi alivyokuwa. Alikuja na kunipigia magoti akiomba msamaha. Alikuwa ni mtu wa kulia tu akikumbuka aliyofanya na akilinganisha hali na mabadiliko ya mtoto aliyonayo. Nilimwelewa na Nikaamua kumsamehe makosa yake, kwani hata kama alikosea na kufanya vibaya sana kwa mtoto lakini moyo wangu ulihitaji na unahitaji kuishi na mama wa mtoto wangu.
 
Back
Top Bottom