Shughuli ipo kwa Pep Guardiola huko Etihad, chama lake la Manchester City limechapwa kwenye mechi mbili mfululizo na sasa kuporomoka hadi kwenye nafasi ya tatu katika msimamo huo, wakiwa na pointi 44, saba nyuma ya vinara Liverpool.
Tottenham Hotspur wapo kwenye nafasi ya pili na pointi 45, huku Chelsea wakikamilisha Top Four na pointi zao 40, huku Arsenal wakiwa kwenye nafasi ya tano na pointi 38 na Manchester United, chini ya kocha wao mpya Ole Gunnar Solskjaer wapo kwenye nafasi ya sita na pointi zao 32. Man United imeachwa nyuma kwa pointi 19 na vinara wa ligi hiyo hadi kufika sasa.