Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

IMG_4410.JPG
 
Mara nyingi ligamenti hii inapata majeraha mara baada ya mtu kuchomoka kwa kasi na kujipinda ghafla au kutua ghafla goti likiwa limenyooka au kujipinda kidogo kama ilivyotokea kwa Bellarin.

Ishara kubwa inayoaishiria nyuzi ya ACL imejeruhiwa ni kusikia mlio fulani ndani ya goti unaojulikana kitabibu kama Popping Sound.
 
Nyuzi ngumu za ACL ziko kama herufi ‘x’ kazi yake ni kuzuia mifupa inayounda ungio la goti kutulia katika eneo lake na isiteleza kwenda upande wa nyuma na vilevile kuliwezesha goti kujizungusha.
 
Ikumbukwe goti lina mijongea mikuu mitatu ikiwamo kunyooka, kupinda kutoka mbele kuja nyuma na kujizungusha. Hivyo basi, uelekeo mwingine wowote nje ya hii huweza kusababisha majeraha.
 
Tukio hili la uwanjani na mtiririko wote mpaka Kocha Unai Emrey kupewa ishara kuwa afanye mabadiliko lilikuwa ni ishara ya mapema kuwa Bellerin amepata jeraha baya hata ya kuchunguzwa kwa vipimo.
 
Back
Top Bottom