Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kumekuwa na wasiwasi Kocha wa Arsenal, Unai Emery amekuwa na matatizo na wachezaji wenye majina makubwa tangu akiwa na PSG wakati alipojikuta katika matatizo na Neymar ambaye alitaka kukaa juu yake.
 
Hata hivyo, Petit anaamini tatizo la Emery kwa Neymar ni tofauti na tatizo la Ozil na anaamini wawili hao hawajakwaruzana isipokuwa Ozil ameshindwa kujituma katika kikosi cha kocha huyo.
 
Kwangu ni rahisi tu. Baada ya Kombe la Dunia wote tunajua kwanini ilisemwa kuwa alicheza vibaya. Ni kwa sababu ya picha aliyopiga na Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan. Lakini kabla ya hapo lini uliwahi kumuona Ozil anacheza vizuri sana uwanjani? Hata kabla ya Kombe la Dunia alikuwa anacheza mechi moja vizuri na nyingine tano vibaya. Ilikuwa hivi kwa miaka miwili iliyopita.
 
Kwahiyo ilianza miaka miwili iliyopita kabla ya Kombe la Dunia. Kombe la Dunia kilikuwa kisu na kwa sababu ni mchezaji anayelipwa zaidi katika timu amekosa kiu na nadhani anasubiri kustaafu,” aliongeza Petit.
 
Habari kutoka ndani ya Arsenal zinadai Ozil aligoma kuondoka Arsenal katika dirisha la Januari huku PSG ikimtaka kwa uhamisho wa mkopo kutokana na kuumia kwa Neymar. Inasemekana Ozil hataki kwenda popote kwa uhamisho wa mkopo na badala yake anaweza kuondoka jumla kama kuna timu itaweza kumlipa mshahara wake mwishoni mwa msimu huu.
 
Ozil aliyesaini mkataba mpya na Arsenal miezi michache kabla ya kuondoka kwa Arsene Wenger analipwa mshahara kwa Pauni 350,000 kwa wiki na dau hilo linadaiwa kuikausha akaunti ya Arsenal huku ikishindwa kununua wachezaji kwa sasa na badala yake imemchukua Denis Suarez kutoka Barcelona kwa dili la mkopo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…