Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Jagielka aliyeanzishwa katika kikosi cha kwanza kuchukua nafasi ya Michael Keane muda mfupi kabla ya kuanza kwa mchezo huo alifunga bao hilo akimalizia mpira wa kichwa wa Dominic Calvert-Lewin akiunganisha mpira uliorushwa na Lucas Digne.
 
Everton ilitangaza Jagielka ataanza dakika 15 kabla ya kuanza kwa mchezo huo akichukua nafasi ya Keane aliyeugua ghafla uwanjani hapo.
 
Everton ilitangaza Jagielka ataanza dakika 15 kabla ya kuanza kwa mchezo huo akichukua nafasi ya Keane aliyeugua ghafla uwanjani hapo.
 
Lakini ilimchukua nahodha huyo dakika 10, tu kufunga bao lake baada ya kutokea maelewano mabaya baina ya safu ya ulinzi ya Arsenal likiwa ni bao lao ka kwanza tangu Aprili 2017 kufunga wakiwa ndani ya eneo la 18.
 
Arsenal itakipiga na Everton kwenye Ligi Kuu England huko Goodison Park leo Jumapili. Mechi muhimu kwa kikosi hicho cha Unai Emery kwani ushindi utawafanya kujiweka kwenye nafasi nzuri zaidi ndani ya Top Four na kuweka hai matumaini yao ya kucheza soka la Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.
 
Wasiwasi mkubwa wa Arsenal ni mechi zao hizo za ugenini. Beki yao imeonekana kuwa ya hovyo hovyo kwenye mechi zao za ugenini kwa msimu huu na hilo linaweza kuwagharimu kwa kiasi kikubwa katika vita hiyo ya Top Four.
 
Kwa msimu huu, Arsenal imecheza mechi 14 ugenini, imeshinda tano tu. Imetoka sare nne na kuchapwa nyingine tano, huku wakiruhusu wavu wao kuguswa mara 27.
 
Kwenye Top Six, wao Arsenal ndio waliofungwa mabao mengi zaidi ugenini kuliko wengine wote, wakiwa na wastani wa karibu mabao mawili kwa kila mechi ya ugenini. Kwenye ligi kwa ujumla, Arsenal wao wapo kwenye tano bora ya timu yenye rekodi mbovu zaidi ya ugenini kwenye mechi za Ligi Kuu England.
 
Arsenal yenyewe imefunga mabao 26 tu. Kwa maana hiyo, wamefungwa mabao mengi kuliko waliyofunga.
 
Kilichopo ni kwamba kwenye mechi zao saba walizobakiza kwenye Ligi Kuu England msimu huu, tano wanacheza ugenini. Mechi zao za ugenini walizobaki Arsenal kwenye ligi msimu huu wakianzia na Everton baadaye leo, watakuwa na kibarua pia cha kuwavaa Watford, Wolves, Leicester City na Burnley. Mechi zao mbili za nyumbani, watawakabili Crystal Palace na Brighton.
 
Rekodi yao hiyo ya mechi za ugenini inawafanya kuwa kwenye wakati mgumu na vita yao ya kufukuzia nafasi ya kurudi kwenye michuano ya kibabe Ulaya baada ya kushindwa hivyo kwa misimu miwili mfululizo.
 
Kwa kifupi tu, kama ukitengenezwa msimamo wa Ligi Kuu England kwa mechi za ugenini tu, Arsenal wangekuwa huko kwenye nafasi ya 10, wakizidiwa na nne ambazo atacheza nazo kumalizia ligi ya msimu huu kama Watford, Palace na Leicester City kwa rekodi hizo za mechi za ugenini. Arsenal wamezizidi Everton, Brighton na Burnley tu kwa rekodi zao ugenini kwa wapinzani wao waliobaki kwenye ligi.
 
Manchester City ndiyo timu yenye rekodi nzuri kwa mechi za ugenini, ikifungwa mabao tisa tu, huku Liverpool wanaochuana nao kwenye mbio za ubingwa, wamefungwa mabao 10. Kwa mechi za nyumbani, Arsenal wapo vizuri sana, wakishika nafasi ya tatu kwa kushinda mechi 14 kati ya 17 ilizocheza huku ikipoteza mara moja tu.
 
Hata hivyo, wakati beki ya kocha Emery ikiwa na rekodi za hovyo, washambuliaji wake wanaonekana kuwa moto zaidi kwenye Ligi Kuu England.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…