Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

LEO Jumanne katika Ligi ya Mabingwa Ulaya pale England ni Liverpool na Porto pale Anfield, halafu Tottenham itacheza na Manchester City lakini homa ya Lionel Messi kutua na Barcelona na kucheza na Manchester United kesho Jumatano Old Trafford ni kubwa zaidi.
 
Messi hajafunga bao lolote katika hatua ya robo fainali kwa mechi 11 zilizopita. Bao lake la mwisho alifunga dhidi ya PSG mnamo mwaka 2013 na tangu hapo mechi za robo fainali hana bahati nazo ingawa amekuwa moto katika mechi nyingi.
 
Sidhani kama tutaweza kumzuia Messi. Inabidi uwe makini na mchezo wako tu. Nadhani inabidi tuicheze mechi kwa ukamilifu mkubwa kama tunahitaji kushinda. Tunajua Messi hapana shaka ni mchezaji bora zaidi duniani katika kizazi hiki na ukiwa akili umeweka kwake tu basi mambo yatakuwa magumu.”
 
Lakini kama tukicheza kitimu, pamoja na ubora wa Messi nadhani tutakuwa na nafasi dhidi yao. Hata hivyo, unahitaji bahati katika hizo mechi mbili. Kama tukiipata bahati hiyo usiku wa kesho, hakuna sababu kwa nini Manchester United isondoke na ushindi wa jumla katika mechi mbili,” aliongeza Yorke.
 
Kocha wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer ambaye alikuwa na Yorke katika kikosi kilichotwaa ubingwa wa Ulaya mwaka 1999 pale Nou Camp huku akifunga bao la pili katika pambano dhidi ya Bayern Munich, Jumamosi alikuwa uwanjani kumtazama Messi na wenzake katika pambano la Ligi Kuu ya Hispania dhidi ya Atletico.
 
Back
Top Bottom