Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

UTAMU wa Ligi ya Mabingwa Ulaya umeshafika hatua ya nusu fainali kwa sasa, ambapo vigogo wanne Barcelona, Liverpool, Ajax na Tottenham Hotspur ndio waliobaki kwenye kinyang’anyiro hicho cha kuusaka ubingwa wa msimu huu.
 
5. Dusan Tadic – dakika 900, mabao 6

Dusan Tadic amekuwa kwenye ubora mkubwa kabisa katika mikikimikiki ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu. Amefunga mabao sita katika dakika 900 alizocheza na kuisaidia Ajax kutinga hatua ya nusu fainali tena wakipita kwenye msitu wenye wababe watupu ambapo imewasukuma nje Real Madrid na Juventus
 
Staa huyo mwenye umri wa miaka 30 hakuonekana kuwa ni wa maajabu alipokuwa kwenye kikosi cha Southampton huko England kabla ya kwenda Ajax, ambako amekwenda kuwa moto na msaada mkubwa kwa msimu huu wakisaka taji la Ulaya.
 
4. Cristiano Ronaldo – dakika 749, mabao 6

Juventus waliwekeza mkwanja mrefu kwa Cristiano Ronaldo ili awasaidie kutamba kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, lakini mambo hayakuwa mepesi kihivyo na kukomea robo fainali wakitupwa nje na Ajax.
 
3. Sergio Aguero – dakika 510, mabao 6

Straika wa Manchester City, Sergio Aguero ameonyesha kuwa mmoja wa washambuliaji matata kabisa duniani kwa sasa baada ya kufunga mara sita kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya licha ya kushindwa kuisaidia timu yake kutinga nusu fainali.
 
Staa huyo wa Kiargentina alifunga bao lake la sita juzi Jumatano wakati Man City ilipotolewa kwa bao la ugenini na Tottenham Hotspur licha ya kushinda 4-3 uwanjani Etihad. Mechi ya kwanza Man City ilifungwa 1-0, hivyo matokeo ya jumla ya 4-4 yaliwapa nafasi Spurs ya kusonga mbele wakitinga nusu fainali. Staa mwingine mwenye mabao sita ni Mousa Marega wa FC Porto
 
2. Robert Lewandowski – dakika 714, mabao 8

Robert Lewandowski kama kawaida yake siku zote amekuwa matata sana anapokuwa mbele ya goli huko kwenye kikosi cha Bayern Munich, ndiyo maana msimu huu amefunga mara nane katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…