Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Vifuatavyo ni baadhi ya vitu ambavyo vimekuwa vinaibua hisia ndani yetu, ambavyo tunapaswa kujihadhari navyo;

Kumbukumbu za utotoni. Utoto ni wakati mgumu sana kwa kila binadamu, ni wakati ambao unataka kupata kila kitu lakini kutokana na mazingira au wazazi uliokuwa nao, kuna vitu ambavyo ulivikosa wakati wa utoto. Huwa unaenda maisha yako yote ukitamani sana kupata vitu hivyo.
 
Na katika utu uzima, akitokea mtu au hali ya kukupa kile ulichokosa utotoni, utamwamini na kukubaliana naye. Mfano watu ambao hawakupata mapenzi mazuri ya wazazi utotoni, huwa inakuwa rahisi kwao kuingia kwenye mahusiano ambayo mwenza wao atampa mapenzi kama ya baba au mama, aliyokosa utotoni.
 
Kupata au kupoteza ghafla. Pale ambapo mtu unapata matokeo mazuri kwa ghafla, au unapoteza kwa ghafla, akili zetu zinaacha kufikiri kwa usahihi, na hapa ndipo tunapokuwa kwenye hatari ya kufanya maamuzi mabovu ambayo yanatugharimu zaidi.
 
Mfano mzuri ni wacheza kamari, akiweka fedha na akapata fedha zaidi, anaamini anajua, hivyo anaendelea kucheza mpaka inafika hatua anapoteza fedha nyingi alizopata. Na anapoliwa fedha alizoweka, anaendelea kucheza, atakuwa tayari kuuza hata nguo alizovaa ili tu aendelee kucheza akiamini ataokoa fedha alizoliwa.
 
Kwenye maisha hali ni hivyo pia, mtu akifanikiwa kwa ghafla anajiona ameshajua kila kitu, anaanza kufanya maamuzi kwenye maeneo ambayo hana uzoefu nayo na anashindwa vibaya. Kadhalika mtu akipoteza ghafla, wengi hukata tamaa na kuona hakuna haja ya kujaribu tena. Tunapaswa kuepuka kufanya maamuzi makubwa mara baada ya kupata au kupoteza kwa ghafla.
 
Shinikizo linalokua. Mara nyingi tunapokuwa na shinikizo fulani ambalo linakua, huwa tunashindwa kufikiri kwa kina na kufanya maamuzi. Ndiyo maana wale ambao wanataka tufanye maamuzi ya haraka yatakayowanufaisha wanatuweka kwenye shinikizo fulani, labda ni muda unaisha, au kitu kinaisha na hivyo tunaona tunapoteza. Epuka sana kuwa kwenye shinikizo lolote lile kama unataka kufanya maamuzi sahihi.
 
Watu wanaochochea hisia. Kuna watu ambao ni mafundi katika kuchochea hisia za wengine. Hawa ni watu ambao ukikaa nao baada ya muda unajikuta ukiwa na hisia kali sana, zinaweza kuwa hisia za furaha, au hisia za chuku kulinga na mapenzi yako kwa mtu huyo au kwa namba usivyompenda. Unapaswa kuwa makini na watu hawa, kwa sababu watakupelekea kufanya maamuzi mabovu. Na wengine wanaibua hisia ndani yako kwa makusudi ili ukosee na wao wanufaike.
 
Watu wanaochochea hisia. Kuna watu ambao ni mafundi katika kuchochea hisia za wengine. Hawa ni watu ambao ukikaa nao baada ya muda unajikuta ukiwa na hisia kali sana, zinaweza kuwa hisia za furaha, au hisia za chuku kulinga na mapenzi yako kwa mtu huyo au kwa namba usivyompenda. Unapaswa kuwa makini na watu hawa, kwa sababu watakupelekea kufanya maamuzi mabovu. Na wengine wanaibua hisia ndani yako kwa makusudi ili ukosee na wao wanufaike.
 
Msukumo wa kundi. Hii ni hali ya juu ya upendeleo wa kundi ambao tumejifunza hapo juu. Kwa kuwa ndani ya kundi, unashawishika kufanya kile ambacho waliopo ndani ya kundi hilo wanafanya, hata kama ukiwa peke yako usingeweza kufanya.
 
Hivi ndivyo watu wanajikuta wakifanya fujo kwa kuwa ndani ya kundi, lakini peke yao wasingeweza. Pia kuwa ndani ya kundi kumekuwa kunaibua hisia ambazo ukiwa nazo mwenyewe huwezi kuwa nazo. Hivyo epuka sana makundi ambayo yanaibua hisia ndani yako ili ufanye maamuzi fulani yanayokugharimu.
 
Ukatibu Mkuu nani alinitoa? Mbona bado naendesha chama kama kawaida tu? Nimegundua the hard way kuwa kuna faida nyingi za kuwa mgumu kuliko hasara. I am in foreva [emoji16][emoji16][emoji16][emoji109][emoji109][emoji109]
Bro hauna uanachama kwa wagumu. Wewe ni chawamita na juzi ulikua nyota tano kusini shahidi Davet
 
Kundi la kwanza ni wale ambao wanaongozwa na hisia katika kufanya maamuzi yao, hawa ni wengi sana na ndiyo wanaojikuta kwenye matatizo makubwa kwao na kwa wengine. Matatizo yote ambayo tunayaona hapa duniani, yamesababishwa na wale ambao wanafanya maamuzi kwa kutumia hisia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…