Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

amber___lulu___BwvDbwwFPmY___.jpg
 
Alan Gilzean na Glenn Hoddle (The Kings of White Hart Lane)

Pale Tottenham kunashangaza kidogo. Mastaa wawili katika nyakati tofauti wamewahi kupachikwa jina la Mfalme. Ilianza kwa mkali wao wa zamani Gilzean ambaye aliwasili klabuni hapo mwaka 1964 akitokea klabu ya Dundee ya Scotland.
 
Hoddle alitisha kwa kipaji chake na hatimaye mashabiki wa Tottenham wakampachika jina la ‘King of White Lane’. Kwa kumbukumbu tu White Hart Lane ni jina la uwanja wa Tottenham ambao ulivunjwa na kujengwa mpya unaotumika sasa wa Tottenham Stadium.
 
Hata hivyo, katika klabu zote hizi ilionekana wazi kwamba Newcastle walimpenda zaidi kwa sababu aliwahi kuwapandisha Ligi Kuu akiwa kama mchezaji, lakini akawapandisha tena akiwa kama kocha. Wenyewe walimpachika jina la King Kev. Wakimaanisha Mfalme Kev. Hadi leo, yeye na Alan Shearer pengine ndiyo watu wanaopendwa zaidi pale St James Park.
 
Henrik Larsson (The King of Kings)

Mtambo wa mabao kutoka Sweden. Mabao yake yalimtambulisha zaidi akiwa na Celtic, kisha Barcelona, kisha Manchester United kidogo. Hata hivyo, Celtic ndipo nyota huyo alikopendwa zaidi. Alifunga mabao 242 kabla ya kuhamia Barcelona kwa uhamisho wa bure mwaka 2004.
 
Ni katika klabu ya Celtic ndipo mashabiki walipompachika Larsson jina la ‘King of Kings’. Walimaanisha kwamba sawa kulikuwa na wachezaji wengi mastaa ambao waliwahi kupita Celtic lakini Larsson alikuwa Mfalme wa Wafalme.
 
Peter Osgood (The King of Stamford Bridge)

Achana na kizazi cha akina Gianfranco Zola. Halafu kikaja kizazi cha akina Didier Drogba, na sasa tuna kizazi cha akina Eden Hazard. Zamani pale Chelsea kuna mtu alikuwa anaitwa Peter Osgood. Mmoja kati ya wachezaji bora wa muda wote Chelsea. Katika kipindi cha miaka 10 aliyocheza Chelsea alikuwa kipenzi cha mashabiki huku akifunga mabao 150 katika mechi 380.
 
Back
Top Bottom