Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

NDUGAI AACHE KUMUHUSISHA MH RAIS NA MIGOGORO YAKE BINAFSI.

Na Thadei Ole Mushi.

Hii ni kwa Mara ya pili Ndugai anajificha na kivuli cha Mh Raisi katika agenda zake binafsi. Mara ya kwanza alifanya hivi wakati akiongea na waandishi was habari kuhusiana na CAG akimtaka CAG aende akajieleze kwa Rais au ajipime mwenyewe angatuke.

Kwa maana Rahisi kabisa Ndugai akishindwa kuumaliza mgogoro wake na CAG akataka Rais auingilie kati yaan akawa anachochea mamlaka za juu ili zimshughulikie CAG.
 
Jana kama ulisikiliza maelezo yake alikuwa anafanya Yale Yale aliyomfanyia CAG. Spika anataka kutengeneza mgogoro kati ya Massele na Rais na massele na Waziri mkuu.

Je Spika wetu hawezi kumaliza migogoro yake mwenyewe bila kutafuta Mbeleko kwa Rais?

Spika amalize migogoro yake binafsi mwenyewe aache kumuhusisha Raisi na migogoro yake. Swala LA CAG alipaswa kulimaliza mwenyewe, hili la Massele alipaswa pia kulimaliza lenyewe.

Anachokifanya Spika bila kujua au kwa kujua anamwongiza Mh Rais kwenye mambo yake binafsi. Halafu ukiangalia migogoro yote Miwili CAG na huu Wa Massele ni migogoro midogo sana ya kukaa Round table tena mkinywa kahawa na kuimalilza. Spika kila Mara anatengeneza taharuki kubwa nchini kwa mambo madogo halafu mwisho wa siku anamhusisha Rais.
 
TUMKUMBUSHE NDUGAI KUWA:-

Kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania Ibara ya 37 Ibara ndogo ya ya kwanza inasema:-

"Mbali na kuzingatia masharti yali yomo katika Katiba hii, na sheria za Jamhuri ya Muungano katika utendaji wa kazi na shughuli zake, Rais atakuwa huru na hatalazimika kufuata ushauri atakaopewa na mtu yeyote, isipokuwa tu pale anapotakiwa na Katiba hii au na sheria nyingine yoyote kufanya jambo lolote kulingana na ushauri anaopewa na mtu au mamlaka yoyote."

Aache kumshauri Rais Mara amwajibishe CAG, Mara Massele hao unaowadanganya ni Mamlaka za uteuzi nk. Mambo yako yaishie ofisini kwako Rais wetu ana mambo makubwa ya kufanya si kuhangaika na migogoro binafsi ambayo haina maana wala tija kwa watanzania.
 
Hifadhi ya Jamii kwa Wakulima yaweza kutatua changamoto nyingi zinazokabili Kilimo Tanzania

Zitto Kabwe, MB

Nimefurahishwa na Uamuzi wa Gazeti la Mwananchi kufanya mjadala Kuhusu sekta ya Kilimo nchini katika Jukwaa la Fikra. Sikuweza kushiriki Katika mjadala huo Kwa sababu za majukumu na haswa kuwa nje ya nchi. Niliona niandike mawazo yangu katika kuchangia tafakari ya namna ya kuleta mabadiliko katika Kilimo. Andiko langu hili ni ufupi wa maandiko yangu kadhaa ambayo nimepata kuandika Kuhusu Kilimo na namna ya kukabiliana na changamoto mbalimbali.
 
Mpango wa Pili wa Maendeleo ya Taifa umeanisha nafasi ya sekta ya Kilimo Katika Uchumi wa Tanzania kwa takwimu hizi. Pia nimeongeza Takwimu kutoka Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa 2018 ili kupata picha kamili ya umuhimu wa Kilimo Katika Uchumi wetu. Baadhi ya Takwimu ni kama ifuatavyo;
 
Sekta ya kilimo inaajiri 67% ya nguvu kazi ya Watanzania. Hii ni Sawa na Watanzania watu wazima milioni 18.
- Sekta ya Kilimo inachangia 30% ya Pato la Taifa (GDP). Hii maana yake ni kuwa Shughuli za Kilimo zina thamani ya Shilingi Trilioni 37 katika Pato la Taifa la Shilingi Trilioni 125.
- Sekta ya Kilimo inaingiza $1.2bn ya fedha za Kigeni kupitia bidhaa zinazouzwa nchi za nje Sawa na 15% ya Mauzo ya Tanzania nje ya nchi.
- Sekta ya Kilimo inalisha 65% ya malighafi za sekta ya viwanda, na
- Sekta ya Kilimo inachangia zaidi ya asilimia 100 ya chakula kinachopatikana nchini kwenye kipindi chenye mvua za kutosha.
 
Jambo kubwa la kung’amua na kutatua katika takwimu hizi ni kuwa Theluthi Mbili ya Watanzania inagawana theluthi moja ya Pato la Taifa. Hii ni changamoto kubwa ambayo inaonyesha sura ya umasikini wa Watanzania na pia inatoa jawabu la namna ya kuondoa umasini:

Kwamba ukiwezesha shughuli za kilimo kuwa na tija na kukua kwa kasi basi utakuwa umekata mzunguko wa umasikini nchini. Eneo mojawapo ninapendekeza ili kuwezesha shughuli za Kilimo kuwa na manufaa kwa Mkulima ni Hifadhi ya Jamii.
 
Hifadhi ya Jamii ni Mfumo imara na endelevu wa kuwajengea uwezo na utayari wananchi katika kukabiliana na matatizo na majanga ya kiuchumi na kijamii. Hifadhi ya Jamii husaidia sana kutoa usalama na uhakika wa kiuchumi, kijamii na kiafya. Kwa namna ilivyo sasa,

Hii ni njia ambayo Serikali, Mwajiri na Mwajiriwa huchangia kiasi fulani cha mapato yake ya sasa kwa ajili ya kumsaidia Mwajiriwa baadaye atakapokuwa hana uwezo wa kupata kipato cha uhakika. Tunachopaswa kufanya ni kumwezesha Mkulima kuwa na njia kama hiyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…