Uzuri hapa huwa hatutukanani. Japo siasa na dini zipo lakini ni kwa kiasi kidogo na tunavumiliana. Tunapokwazana tunawekana kwenye iginoa listi halafu baadaye tunasameheana na mambo yanasonga mbele. Hapa kuna watu wa kila aina - wasomi, matajiri, wajasiriamali, wakulima na wajuzi wa kila mambo. Kiumri kuna vijana wa kuanzia miaka 16 mpaka wazee wa miaka 80 (mimi). Ukiangalia kwa juu juu utadhani kuwa ni uzi wa hovyo hovyo tu lakini ukikaa kwa muda utagundua kuwa kumbe JF yote iko hapa.
Karibu sana
Min 92.
(Na mimi ndiye mtunza kumbukumbu na mafaili yote ya uzi huu. Ukitaka kujua jambo lolote hapa niulize)