Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

.
image_search_1559852664657.jpeg
 
Sheria zao zinasemaje kuhusu mtu anayestahili kudunguliwa, kibaka,jambazi, mgoni wako, jirani yako aliyefungulia sauti kubwa ya mziki au anayetaka kukupora baamedi wako
Florida kule kuna sheria ya "Stand Your Ground". Maana yake hakuna kutishiwa nyau. Ukihisi tu kuwa umetishwa basi una haki ya kumshindilia mtu shaba upendavyo. Kibaka, jambazi, mgoni na ye yote kama unaamini amekutishia maisha yako basi ni halali kummiminia shaba. Jirani yako akifungulia muziki kwa sauti kubwa unaweza kumuitia polisi ila ukijifanya kimbelembele ukaenda kwake kumuomba apunguze sauti; na akahisi kuwa pengine umeenda kumpa kichapo au kumuua basi anaweza akakuwahi wewe na kukumiminia risasi. Huwezi kujua yupi ana bunduki na yupi hana. Ndo maana kila leo visa vya watu kulimana shaba haviishi.
 
Back
Top Bottom