Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

OLE Gunnar Solskjaer ameshusha onyo kali kwa mchezaji wake Jesse Lingard kutuliza akili yake na kucheza mpira kama kweli anataka kuendelea kubaki kwenye kikosi hicho cha Old Trafford.
huyo lingard bora aondoke, mpira umemshinda nadhani kazi pekee inayomfaa kwa sasa ni kuwa baharia atakayewapa huduma vijukuu vya malikia
 
Ujumbe kama huo umetumwa pia kwa mshambuliaji mwingine wa timu hiyo, Marcus Rashford kwamba kama wanataka kubaki kwenye kikosi, basi wacheze mpira na si kufikiria mambo mengine ya huko uswahili.
Onyo hilo la Solskjaer limeungwa mkono na msaidizi wake Mike Phelan, ambaye amesisitiza kwamba anataka wachezaji hao wawili kuweka adabu na kuwa na nidhamu bora kwenye vyumba vya kubadilishia.
 
Solskjaer na Phelan waliripotiwa kuwa na mjadala tofauti kidogo kuhusu Lingard alipoamua kuzindua nembo yake binafsi ya mavazi ya "Be Yourself" Krismasi mwaka jana. Nembo hilo itakuwa sehemu ya kampuni yake staa huyo inayofahamika kama JLINGZ, ambayo pia imekuwa ikihusisha na dawa za kunyoa na kava za iPhone.
Mabosi wa Man United sasa wanashawishika kwamba Lingard amekuwa haweki mkazo wa mambo ya uwanjani ili kuwa mchezaji bora na badala yake amekuwa akiandamwa na mambo mengine kibiashara.
 
Jambo hilo limedaiwa kumwaathiri Rashford, ambaye ni swahiba wake mkubwa. Rashford amedaiwa kushindwa kutuliza akili yake uwanjani hasa kwa msimu huu ambapo amefanywa kuwa chaguo la kwanza kwenye nafasi ya ushambuliaji.
Lingard alizindua nambo yake hiyo ya mavazi Desemba mwaka jana, wiki moja kabla ya kwenda kucheza mechi Anfield, ambako walichapwa 3-1 na kumfanya kocha Jose Mourinho kufutwa kazi huko Old Trafford.
Nahodha wa zamni wa Man United, Roy Keane aliponda sana uamuzi wa Lingard kwenda kuzindua mavazi kwenye wiki ya mechi muhimu dhidi ya Liverpool.
 
Jambo hilo alilizungumzia pia Gary Neville, aliyesema hana shida na mavazi hayo, shida yake ipo kwenye kipindi cha uzinduzi.
“Ukweli ni kwamba kabla ya mechi ya ugenini kwa Liverpool, mechi kubwa kabisa ya msimu, siwezi kuzindua nembo ya mavazi. Nisingefanya wiki hiyo, ningetuliza akili yangu kwenye mechi ya Liverpool, sitaki stresi wala sitaki usumbufu,“ alisema Neville.
 
Lingard alifunga kwenye mechi hiyo, lakini baada ya hapo, hajaona utamu wa kufunga, huko mechi zote alizocheza msimu huu hajafunga hata bao moja. Rashford kwa upande wake amefunga mabao mawili kwenye ule ushindi wa 4-0 katika mechi ya kwanza dhidi ya Chelsea na baada ya hapo alitoka patupu hadi juzi Jumamosi alipofunga kwa mkwaju wa penalti dhidi ya Leicester City huko Old Trafford.
 
😂😂😂 akienda kukojoa anapouse
nikupe kali ya leo.
znz kuna shamba fulani ukienda utakutana na kilima flani kinaitwa kilima nyege.
bwana weeee kuna kiongozi fulani mkubwa sana ambaye kwa sasa ni mstaafu kutoka huko kwenu utanganyikani aliwahi kupitishwa hiyo barabara.

kuna hisia fulani za ajabu zilimjia bada ya kupitishwa kwenye hicho kilima jambo lililopelekea asimamishe msafara na kumtaka dereva wake arudishe tena gari nyuma ili apite kwa mara nyengine tena kwenye kilima nyege.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]team CR7

#HivyomandevuAkome
#AnatattooKamaUkutaWaChooChaShuleYaMsingiYaSerikali
Mimi naomba tuishie hapa.
team messi mupo wangapi humu ndani?
kabla hamjapambana na mimi naomba mujikusanye kwanza kama kuna mchango wa harusi wa familia
 
Back
Top Bottom