Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Taarifa za kutoka huko Emirates zinafichua kwamba Arsenal itajiweka kwenye hatari ya kupoteza huduma ya mastaa wake wa nguvu, Pierre-Emerick Aubameyang na Alexandre Lacazette kama tu watashindwa kukamatia tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao. Huu ni msimu wa tatu mfululizo, Arsenal wameshindwa kuwamo kwenye michuano hiyo ya Ulaya kwa kushindwa tu kumaliza ligi ndani ya Top Four.
 
Hivi karibuni, Arsenal ilitumia Pauni 75 milioni kunasa huduma ya Nicolas Pepe, lakini bado haijawasainisha dili ndefu Lacazette na Aubameyang na taarifa zinadai kwamba wachezaji hao wanasubiri kwanza kuona kama timu itacheza kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya mwakani.
 
Kwa sasa, supastaa huyo yupo Juventus. Ikiwa hana hata misimu mwili, Juventus tayari wame shaanza kuhaha kutafuta mrithi wake. Anakopita Ronaldo ni janga. Shughuli yake anafanya ndani ya uwanja kwa ajili ya timu, ngumu sana kupata wa kuziba pengo lake pindi anapoondoka.
 
Real Madrid nao wanafahamu wanachokikosa kwa sasa, ikiwamo pia La Liga ambao wanaamini kuondoka kwa supastaa huyo wa Kireno kumeacha pengo kubwa kwenye soka la nchi hiyo. Juventus wameliona hilo mapema na sasa wanahaha sokoni kutafuta mtu wa kuja kuvaa buti zake atakapoondoka Turin.
 
Mabingwa hao wa Serie A wametenga kitita cha Pauni 335 milioni kwa ajili ya kunasa mastaa hao, Mo Salah na Mbappe kwenye fowadi yao, pia wakiwafikiria wakali wengine, Son Heung-min, Toby Alderweireld na Christian Eriksen ili kuboresha kikosi chao na kukifanya kuwa na nguvu zaidi ya kufanya kweli kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.
 
Ronaldo akiondoka Juventus, jambo hilo litazigusa timu nyingi kuhofia kupoteza mastaa wao, hasa PSG ambao Neymar na Mbappe wanaweza kuwekwa kwenye mpango wa kwenda kuziba pengo lake huko Turin, lakini kwa Ligi Kuu England, Mo Salah wa Liverpool na Harry Kane wa Tottenham Hotspur wanaweza kuhusishwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…