Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Salah aliuelezea mpango huo wa Newcastle United kuwa ni uhamisho wa ndoto zake. Lakini, klabu hiyo ya Misri kutaka ilipwe ada ya mkopo ya Pauni 500,000 iliwafanya Newcastle kutoweka na kuachana na mpango wa kumsajili Mo Salah, ambaye alikuja kunaswa na FC Basel mwaka uliofuatia.
 
Luka Modric – Newcastle United

Mwaka 2008, Kevin Keegan, akiwa kocha wa Newcastle United kipindi hicho, alipokea simu kutoka kwa wakala wa kiungo Luka Modric akiomba mchezaji huyo aende akakipige kwenye kikosi hicho cha St James’ Park.
 
Kipindi hicho, fundi wa mpira Modric alikuwa anakipiga kwenye kikosi cha Dinamo Zagreb na wakala wake alitaka aende akajiunge na Newcastle United, ambayo si mchezo miaka hiyo ilikuwa moja ya timu nzuri za kuzitazama kwenye Ligi Kuu England.
 
Zinedine Zidane – Blackburn Rovers

Baada ya kushinda ubingwa wa Ligi Kuu England mwaka 1995, mwenyekiti wa Blackburn Rovers, Jack Walker alimuuliza kocha wa kikosi hicho kwa wakati huo, Kenny Dalglish kama anamtaka Zinedine Zidane basi waende kumsajili.
 
Lakini, mwenyekiti huko, Walker baadaye alijikuta tu akiingia kwenye vitabu vya kumbukumbu kwa kuamua kubeza mpango wa kumsajili Zidane, akidai kwamba unawezaje kufanya usajili wa kiungo huyo Mfaransa wakati kwenye kikosi yupo Tim Sherwood. Kwa mtazamo wa mwenyekiti hiyo, kipindi hicho Sherwood alionekana kuwa staa kuliko Zidane.
 
Roberto Carlos – Aston Villa

Gwiji wa Kibrazili, Roberto Carlos alimvutia mwenyekiti wa Aston Villa, Doug Ellis wakati huo kwenye mechi ya kirafiki kati ya Brazil na Sweden iliyopigwa kwenye Uwanja wa Villa Park mwaka 1995.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…