Mkuu wazazi wako wameona mengi na wanaona kesho yako itakuwa ya mashaka......
1. Je baba wa mtoto yupo hai?
2. Je Anakaa mkoa huohuo na je wanamawasiliano?
3. Je wanawasiliana kwaajili ya mtoto na jibu lako kaka hapana je unauhakika??
4. Sababu zipi zilipelekea huyo binti na mzazi mwenzie kutokuwa pamoja? kama ni hali ya maisha je huyo mwamba akipata maisha mazuri huoni utaachwa katika mataa?
5. Ulikutanaje na huyo bibie? Na ulimkuta katika hali gani? Elekea ulimkuta katika hali ambayo alihitaji any man amfariji nawewe ukadhani upendo..so akiwa sawa na baba watoto akirudisha majeshi atakubwaga.
6. Je unaweza stahimili kupokea dharau na maneno ya shombo kutoka kwa huyo bibie pindi baba watoto akijirudi (je hautojidhuru?)
7. Kipi kinafanya uamini kuwa huyo mpenzi wako atakuwa the best choice among other women?
8. Upo tayari Kuvumilia na kufa ndani kwa ndani bila kuwaeleza wazazi wako pindi binti akichange na kukuacha dillema?
Nina X wangu ni kama single maza maana baba wa mtoto yupo mbali ila huwa wanawasiliana sana tu... Sasa nikiwekaga tu kipicha cha mwanamke mwingine hata kama ni birthday wishes nae atamtafuta baba wa mtoto atarecord video ataweka status na hapo unaangalia macho yake mekuuuundu na anaonesha kachoka Hahahahahaha ila huwa nachukulia simple maana naonaga kama ana mental disorder