Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

UHURU WA ZANZIBAR
Manamo saa sita na dakika moja za usiku wa kuamkia taarikhi 10 Disemba 1963, bendera nyekundu tupu iliteremshwa kutoka kwenye mlingoti wake na Bendera ya Dola Huru ya Zanzibar yenye karafuu mbili ilipandishwa na kupepea katika mlingoti uliokuwepo kwenye ardhi ya nchi katika uwanja wa Mivinjeni (Coopers Insititute), uwanja huo hivi sasa ati unaitwa "Uwanja wa Maisara".

Tafauti na koloni nyengine za Muingereza, Zanzibar haikuwepo bendera ya Kiingereza kuteremshwa, kwa sababu haikupatapo kupepea juu ya ardhi ya Zanzibar. Japokuwa ilitiwa chini ya himaya ya Kiingereza, haikuwa koloni kama vile koloni nyenginezo za Kiingereza, Zanzibar haikusita kuwa Dola kwa muda wote huo.
 
[emoji23][emoji23][emoji23]Glory Glory Manchester united
Nilishajua mnapokwama Manchester.
Mna goalkeeper mrembo Sana aisee[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Nlikuwa najiuliza hivi kwanini kila siku mnafungwa!?!Sasa kwa goalkepeer huyu msipigwe kweli[emoji23]
Dah, Manchester hamsinii,, Manchester Ni bureee[emoji1787][emoji1787]
 
YAITWAYO "MAPINDUZI"
Mafisadi wachache kwa ajili ya maslahi ya nafsi zao hawakutahayari kuchanganyika na wageni waliyokuwepo ndani ya nchi na waliyoletwa kutoka nchi za jirani kwa makusudio khasa ya kuivamia Zanzibar na kuiondoa Serikali ya wananchi. Wananchi mafisadi hao walikubali kuongozwa na wageni, 33 John Okello aliyetoka kwao Uganda, Injin aliyetoka kwao Kenya na Mfaranyaki aliyetoka kwao Tanganyika, kuivamia nchi yao katika usiku wa manane wa kuamkia taarikh 12 Januari 1964. Wananchi, mafisadi kwa sababu ya maslahi ya nafsi zao hawakuhisi uchungu kuipoteza nchi yao, wala kuzipoteza roho za wazee wao, za ndugu zao na za marafiki zao.
 
Kwa mujibu wa kitabu cha huyo aliyejipa ujamadari wa hayo 'mavamizi' ya Januari 12, 1964, John Okello, amesema kuwa watu waliyokufa katika 'mavamizi' hayo ni 13,000. Hii ni idadi ndogo kabisa aliyopenda kuitaja. Ukatili, ushenzi na unyama uliofanywa katika visiwa hivi vilivyokuwa na ustaarabu wa kupigiwa mfano, hauwezi hata kuhadithika. Wengi waliokuwa wanaijua Zanzibar, waliona taabu kuyaamini waliyokuwa wameyasikia yametokea Zanzibar kutokana na hayo yenye kuitwa 'mapinduzi'.
 
Ilifika hadi, siku hiyo ya 'mavamizi' majahil na makatili hao kuwanajisi maiti wa kike. Kitendo hicho hakijapatapo kufanyika katika nchi nyingi ulimwenguni zenye ubinaadamu na ustaarabu wake. Lenye kuzidi kushangaza na kusikitisha ni kumsikia mwananchi mwenye kujulikana kuwa yeye ndiye mwongozi wa hao wenye kujiita "progressives" akasema kuwa, watu waliyouliwa katika hayo yenye kuitwa 'mapinduzi' ni 491! Oh! Mwenyewe Okello alieongoza hayo mauwaji amesema kuwa wamekufa wananchi 13,000.
 
La kustaajbisha zaidi ila pale inapojulikana kuwa haya yote yalipangwa kabla ni kuwa kwa siku 30 tu yaaani Desemba 10 mpaka Januari 11 ilitosha kujuwa uovu wa Serikali hata ikastahiki kupinduliwa? Hata ingelikuwa ni ovu hivyo, bali njia za kuiondowa za kikatiba zilikuwepo ambazo zingaliweza kutumika, khasa na hao Wapinzani. Haikuhitaji hata kidogo kutumia nguvu. Lakini hakika khasa ni kuwa mambo yalikwisha pangwa zamani, haya ni matekelezo tu!!
 
KUULIWA KWA MUHSIN, SULEIMAN NA AHMED
Siku ya taarikhi 13 Januari 1964, siku moja baada ya hayo yenye kuitwa "mapinduzi" kufanyika, wapendao kujiita "progressives", Makomred, waliwachukua vijana watatu, Muhsin Badr, Suleiman Badr na Ahmed Suleiman kutoka katika kituo cha Raha Leo, kikiwa kimoja kati ya vituo vilivyo kuwa vimewekwa na wakuu wa mavamizi ati kwa ajili ya kuhifadhi usalama wa wananchi.

Baada ya kuwaondoa hapo, waliwafunga kamba za mikono na kisha waliwafunganisha nyuma ya lori na kuwaburura kutoka Raha Leo mpaka Chukwani kiasi ya mwendo wa maili tano au sita, na huku njia nzima vijana hao walikuwa wakiteseka kwa kujipiga na mawe, kuchomwa na visiki vya mijiti, vigae na kujipiga na majiti ya njiani.
 
Walipofika huko Chukwani walikuwa si wahai si maiti, bali walikuwa badi wakitweta. Juu ya hali kama hizo walizokuwa nazo wananchi hao katika wakati huo, midhalimu ati "progressives" walianza kwanza kuwasubu kwa kuwatukana na kwa kuwaambia maneno machafu machafu, na mwisho waliwauwa kwa kuwapiga risasi. Kisha waliwachimbia shimo na kuwafukia wote pamoja. Hayo yaliweza kujuulikana kutokana na kujisifu kwao wenyewe hao madhaalimu. Wakati utafika ikiwa watanusurika katika ulimwengu huu, kattu hawatanusurika katika ulimwengu ujao. Watalipwa kwa kila walilokuwa wamelitenda, na hivyo ndivyo itavyokuwa kwa kila mwenye kutenda mema na maovu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…