Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Hahaha sawa, ila hilo jina nililipata kwa binti mmoja sijui msukuma yule mtoto? Alikuwa mzuri balaa, ana kasura fulani hivi karefu, alikuwa mwembamba ila ana shepu matata, mpoleee yaani nilikuwa nampenda sana japo sikuwa na mazoea nae sana nilikuwa tu namuona kanisani. Amesababisha hadi nalipenda hilo jina yani

Sent using Jamii Forums mobile app
Yuko wapi sasa hivi huyo Mlimbwende? Hilo jina ni common kwa Wazanaki na Wajita. Sina uhakika sana kama Wasukuma wanalitumia. Mwambie Huyo mtoto kaka yake namtafuta. 😁 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
1585082965172.png


Baraza la Mawaziri la mwanzo la baada ya uhuru wa Zanzibar.
 
Yuko wapi sasa hivi huyo Mlimbwende? Hilo jina ni common kwa Wazanaki na Wajita. Sina uhakika sana kama Wasukuma wanalitumia. Mwambie Huyo mtoto kaka yake namtafuta. [emoji16] [emoji2089][emoji2089][emoji2089]
Hahaha kama wewe kaka yake utakuwa unajua alipo maana tayari ulishakula mahari tangu mwaka juzi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwaka 2002 Fujitsu walianza kutengeneza za mkononi zinazoitwa iPAD, 2010 Apple wakatengeneza iPad. Kutokana na majina kufanana ilibidi Apple wanunue haki ya jina kutoka Fujitsu kwa dola milioni 4.
Mwaka 2018, Apple wameingiza dola bilioni 18.8 kupitia mauzo ya iPad pekee.
Chanzo:AppleInsider & Statistica
 
Mieleka ni mchezo wa Maigizo lakini yenye Uhalisia. Kwa kila kinachofanyika kinakuwa Kimepangwa tayari na Wapiganaji Wanajua, Lakini Unachokuwa Unakiona Kinafanyika Kwa Uhalisia ndio maana Watu huumia. Kwa Ufupi "Mieleka Wanakuonesha Kile Wanachotaka Uone na Sio uhalisia wa kinachotokea.
 
Moja ya anguko kubwa sana la kibiashara kuwahi kutokea Duniani, ni kutoka Kampuni ya Nokia.

Jifunze kitu, Mwaka 1998 Nokia alitajwa kuwa kampuni kubwa ya Simu za mkononi Duniani. Mwaka 2003,Walitoa simu ya "Nokia 1100" ambayo ilitajwa kuja kuleta mapinduzi makubwa katika Ulimwengu wa Simu na kweli ilinunuliwa Haswa (SWIPE KUIONA) na mpaka sasa ndio Brand ya Nokia ambayo imenunuliwa zaidi kuzidi zingine... Lakini hapa ndipo matatizo yalianzia...Kivipi? Ni hivi...

Wakati Apple wanatoa simu ya iPhone toleo la kwanza mwaka 2007, asilimia 95 ya simu zote duniani zilizokuwa zikitumiwa na watu zilikua ni Nokia.

Lakini Chaajabu ni baada ya Miaka 5 mbele Thamani ya Nokia ilishuka kwa takribani asilimia 90, na mwaka 2013 Microsoft waliinunua Nokia hapo ndio Wakazidi kujizika zaidi.

Kuna kitu Tujifunze, Kilichowaangusha Nokia ni Kubweteka na Sifa kemkem Walizokuwa wakipewa, Walijiona wao ndio bora na hakuna Kampuni yoyote ingeweza Kuwapindua hivyo Walikosa kuendana na Soko Kwa kushindwa kuleta Ubunifu mzuri kwa Haraka Na Chaajabu zaidi katika Kampuni ambayo hata hawakuifikiria au Haikufikiriwa ingeweza kufanya Maajabu katika Upande wa Simu ni Apple.

Sababu wao walionekana kuwa wapo upande zaidi wa Comouters na iPod.. Lakini kilichowatokea hawatokaa Kuamini mpaka sasa.

Wakati wanastuka kutoka Usingizini, ilikua tayari hali imebadilika licha ya kujitahidi kufanya mabadiriko kadhaa Bado hali kwao imekuwa ngumu.

Mambo yanaweza kubadirika kwa haraka sana zaidi hata unavyofikiria, Hakuna Muda wa kupoteza. Hakikisha Unapambana kikamilifu kwa nguvu sana, Sababu Wakati wewe unafurahia Mafanikio yako, Kuna mtu yupo Chini Anapambana Afikie Mafanikio tena katika Jambo ambalo wewe Pia Unafanya.

Acha Kuutumia UBONGO wako katika mambo yasiyofaa, Hakikisha kila siku unakuwa mtu mpya.
 
Kwenye Game of Thrones na ASOIAF, kitu kirefu zaidi ni mnara wa Hightower uliopo Oldtown, The Reach, siyo ukuta wa kaskazini (The Wall)
Mnara wa Hightower una urefu wa futi 800.
Wakati ukuta una urefu wa futi 700.
Chanzo:A wiki of ASOIAF & Fandom
 
Tendo la ndoa linamfanya mwanamke awe na mvuto zaidi. Homoni ya oestrogen huongezeka kadri mwanamke anavyofanya mapenzi, homoni hiyo licha ya kazi nyingine nyingi mwilini inaifanya ngozi iwe nyororo na inalainisha nywele.
Chanzo:WebMD
 
Kentucky, Marekani: Dr Amanda Hess alikuwa amelazwa hospitali akiwa anakaribia kujifungua. Alisikia mwanamke mwenzake humo wodini ameshikwa na uchungu na hapakuwa na daktari, akaenda kumsaidia kujifungua kisha akarudi kwenye kitanda chake. Baadae siku hiyohiyo na yeye akajifungua.
Chanzo:WashingtonPost
 
The Great Emu War: Mwaka 1932 jeshi la Australia lilipigana vita na ndege aina Emu ambao hawawezi kupaa. Ndege hao walikuwa wanaharibu mazao ya wakulima. Inachukuliwa kuwa ndege hao walishinda vita kwa sababu waliendelea kuwepo na kusumbua wakulima lakini hakuna mwanajeshi aliyekufa. Vita hiyo ilidumu kwa siku 38.
Chanzo:Wikipedia.
 
Back
Top Bottom