Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

"Katika hostel zile watu tunaowaleta lazima liangaliwe upya, hakuna sababu ya mtu anakaa pale siku 14-20 wakati unamuona kabisa hana tatizo, tu concetrate zaidi na wagonjwa, kuendelea kuwahifadhi watu ambao ni wazima, tunapoteza resources zetu" - Rais Magufuli
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 22 Aprili, 2020 amezungumza na Viongozi Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama akiwa Chato Mkoani Geita kuhusu hali ya ugonjwa wa homa ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona (Covid-19).
Mhe. Rais Magufuli amewashukuru Watanzania kwa kuitikia wito wa kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Corona, na kwa kushiriki katika siku 3 za kumuomba Mwenyezi Mungu aepushe janga la ugonjwa huo.
Mhe. Rais Magufuli amewapongeza Madaktari na Wauguzi walio mstari wa mbele katika kutoa huduma za matibabu kwa wagonjwa wa Corona na ametoa wito kwa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kuhakikisha inachukua tahadhari za kutosha kwa misaada ya vifaa vya uchunguzi wa Corona na vifaa vya kujikinga kuambukizwa au kuambukiza (barakoa) hasa baada ya baadhi yake kuhofiwa kusababisha maambukizi ya ugonjwa huo.
Pia ametoa wito kwa wenye viwanda hapa nchini kuzalisha barakoa kwa ajili ya Watanzania na vifaa vingine vya kukabiliana na ugonjwa huo yakiwemo mavazi ya watoa huduma na mashine za kupumulia kwa wagonjwa badala ya kutegemea vifaa hivyo kutoka nje ya nchi pekee.
Mhe. Rais Magufuli amewataka viongozi kujihadhari na baadhi ya njia zinazotumika kukabiliana na ugonjwa huo, ikiwemo kupulizia mitaa na majengo kwa kutumia kemikali zisizokuwa na uwezo wa kuua virusi vya Corona kama ilivyofanyika kwa baadhi ya Mikoa hapa nchini, na badala yake amewataka viongozi hao kusisitiza njia za uhakika za kujikinga na ugonjwa huo.
Aidha, Mhe. Rais Magufuli amesema Serikali haitawafungia wananchi majumbani (lockdown) wala kulifunga Jiji la Dar es Salaam ili kuepusha madhara makubwa yanayoweza kuwakumba wananchi na kuathiri uchumi wa nchi, na ametaka Watanzania kuondoa hofu, kuendelea kuchukua tahadhari huku wakiendelea na shughuli zao za uzalishaji mali na ujenzi wa Taifa.
“Tuwaondoe hofu wananchi, sio ugonjwa huu pekee unaosababisha vifo kwa wananchi, na sio kila anayepoteza maisha hivi sasa basi amekufa kwa Corona, nimejulishwa takwimu za mpaka jana idadi ya walioambukizwa ni 284 na kati yao takribani 100 wamepona, tuwaambie wananchi kuhusu taarifa hizi badala ya kuwaacha wanajawa na hofu hali.
 
"Benki ya Dunia najua wametoa ofa ya nchi zinazosumbuliwa na Corona kukopa pesa, badala ya kukopesha tena, wasamehe madeni kwa nchi hizi, mfano sisi huwa tunalipa karibu Bil 700, watusamehe ili hizi pesa zikatumike kupambana na hili janga" - Ameyasema Hayo Magufuli
 
Kwakweli mgeni kama ataondoka ni jambo la kutia moyo.
Mnisamehe kwa kudandia treni ya kwenda unguja[emoji1787][emoji1787]
 
Pamoja na lawama zote, naomba mnisamehe, mi namuunga mkono mia kwa mia mh rais.
Tupambane na korona katika hali kama ilivyo.
Ushauri wangu kwa serikali waweke ruzuku kwenye vifaa vya kujilinda kama barakoa na vitakasa mikono ili kuwepo na bei wezeshi kwa kila mtanzania

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…