Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Usiku wa juzi kama kitambo cha saa 7 hivi nikiwa mitaa ya Kariakoo Dsm nilijionea matukio yaliyoniacha mdomo wazi.
Watu wamekusanyika kwenye vijiwe vya kahawa kwenye makundi makubwa, wakiwa wamekaribiana umbali nchi 6 tu wanapiga stori huku wakipata kahawa bila tahadhali yoyote.
Watu wanapiga stori huku wakicheka na kushikana mikono wakipeana tano.
Daaa, niliumia sana.
Nadhani watalaam wa afya wa serikali wapite shule ya uhuru kuanzia saa 3-8 usiku waojionee hatari ilivyo
Afadhali tusahau corona kidogo...
Kaa umbali wa mita moja na mwenzako!!
 
Nimeipenda sana hotuba hiyo, ingawa siyo lazima wengine wakubaliane naye
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 22 Aprili, 2020 amezungumza na Viongozi Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama akiwa Chato Mkoani Geita kuhusu hali ya ugonjwa wa homa ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona (Covid-19).
Mhe. Rais Magufuli amewashukuru Watanzania kwa kuitikia wito wa kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Corona, na kwa kushiriki katika siku 3 za kumuomba Mwenyezi Mungu aepushe janga la ugonjwa huo.
Mhe. Rais Magufuli amewapongeza Madaktari na Wauguzi walio mstari wa mbele katika kutoa huduma za matibabu kwa wagonjwa wa Corona na ametoa wito kwa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kuhakikisha inachukua tahadhari za kutosha kwa misaada ya vifaa vya uchunguzi wa Corona na vifaa vya kujikinga kuambukizwa au kuambukiza (barakoa) hasa baada ya baadhi yake kuhofiwa kusababisha maambukizi ya ugonjwa huo.
Pia ametoa wito kwa wenye viwanda hapa nchini kuzalisha barakoa kwa ajili ya Watanzania na vifaa vingine vya kukabiliana na ugonjwa huo yakiwemo mavazi ya watoa huduma na mashine za kupumulia kwa wagonjwa badala ya kutegemea vifaa hivyo kutoka nje ya nchi pekee.
Mhe. Rais Magufuli amewataka viongozi kujihadhari na baadhi ya njia zinazotumika kukabiliana na ugonjwa huo, ikiwemo kupulizia mitaa na majengo kwa kutumia kemikali zisizokuwa na uwezo wa kuua virusi vya Corona kama ilivyofanyika kwa baadhi ya Mikoa hapa nchini, na badala yake amewataka viongozi hao kusisitiza njia za uhakika za kujikinga na ugonjwa huo.
Aidha, Mhe. Rais Magufuli amesema Serikali haitawafungia wananchi majumbani (lockdown) wala kulifunga Jiji la Dar es Salaam ili kuepusha madhara makubwa yanayoweza kuwakumba wananchi na kuathiri uchumi wa nchi, na ametaka Watanzania kuondoa hofu, kuendelea kuchukua tahadhari huku wakiendelea na shughuli zao za uzalishaji mali na ujenzi wa Taifa.
“Tuwaondoe hofu wananchi, sio ugonjwa huu pekee unaosababisha vifo kwa wananchi, na sio kila anayepoteza maisha hivi sasa basi amekufa kwa Corona, nimejulishwa takwimu za mpaka jana idadi ya walioambukizwa ni 284 na kati yao takribani 100 wamepona, tuwaambie wananchi kuhusu taarifa hizi badala ya kuwaacha wanajawa na hofu hali.
 
Hilo pia nalikubali.
Asante sana mh rais
"Benki ya Dunia najua wametoa ofa ya nchi zinazosumbuliwa na Corona kukopa pesa, badala ya kukopesha tena, wasamehe madeni kwa nchi hizi, mfano sisi huwa tunalipa karibu Bil 700, watusamehe ili hizi pesa zikatumike kupambana na hili janga" - Ameyasema Hayo Magufuli
 
Mbali na kuwa na virutubisho vingi kitunguu saumu pia kina dutu/kemikali adhimu ambazo zina uwezo wa kupambana na vimelea vya maambukizi ya magonjwa na pia kemikali hizo zina uwezo wa kubadili au kuiga utendaji kazi wa dutu nyingine za mwili jambo ambalo jambo linalofanya kitunguu saumu kuwa moja ya mitishamba bora zaidi katika kutibu matatizo mbalimbali ya afya.
 
Nguvu ya kutibu ya Kitunguu saumu inatokana na kuwa na kemikali tiba zifuatazo;
Allicin
Alliin
Alliinase
Scordinins
Selenium
Vitamins(A,B,C and E)
Uwepo wa kemikali hizi katika kitunguu saumu kunafanya kitunguu saumu kuwa na uwezo wa kutibu matatizo yafuatayo.
 
Back
Top Bottom