Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kuoa au kuolewa na kuwa na watoto,kuwa na sehemu ya kuishi na kuwa na gari la kutembelea ni mahitaji ya muhimu kwa mtu mzima. Ni mahitaji ya lazima. Kutimiza mahitaji haya hayategemei kuwa na ndoto kwa mtu. Ndiyo maana,hakuna mtu wa kukuuliza unataka kufanya nini,na kumjibu kuwa,nataka kuwa na watoto au nataka kujenga nyumba. Nyumba,watoto na kuoa ni mahitaji ya msingi kwa binadamu aliyekamilika na mtu mzima.
Exactly.
 
Dunia haitakukumbuka eti kwa kuwa ulijenga nyumba. Kama ni nyumba kila mtu anaweza kujenga. Na wengine wanazo nyingi kila sehemu. Jamii haitakukumbuka kwa kuwa ulioa na kuzaa watoto wengi. Kila mtu anao wake na watoto wa kutosha. Tena wengine wanao hata wake wanne. Hakuna mtu atakukumbuka eti ulinunua gari. Kuna watu wengi sana wana magari zaidi yako na ya kutosha.

Ndoto kuu za maisha ni kusudi la maisha yako. Ni jumla ya maisha yako yote. Ndoto kuu ya maisha ndiyo utaifanyia kazi maisha yako yote. Kuitimiza ndoto kuu ya maisha,unapaswa kuifanyia kazi kila Siku mpaka mwisho wa safari yako. Kutimiza ndoto kuu lazima ufanye kwa bidii.
Thanks.
 
Ndoto kuu za maisha yako ni jumla ya maisha yako.Kile unachofanya lazima kikutambulishe duniani. Ukifa Leo,utaacha alama gani!? Nyumba? Gari? Watoto? Mke? Mume? Au utaacha nini? Kama hujawa na ndoto ya kuwa na alama,anza kufikiria upya malengo yako na ndoto kuu ya maisha.

Mpendwa,usiseme, kwa umri ulionao mkubwa huwezi kutimiza. Usiseme kwa umri wako wewe usiseme umechelewa. Ndoto kuu ya maisha haina muda maalum wa kutimia. Kuna watu wengine wanaweza kuziishi ndoto zao na kuzitimiza wakiwa vijana,wengine wakiwa na umri wa kati na wengine wanaweza kutimiza wakiwa wazee. Hii ina maana kuwa kutimiza ndoto kuu ni muda wote wakati bado unaishi. Ni jumla ya maisha yako yote. Kama bado unaishi,bado unao muda wa kutimiza ndoto kuu haijalishi umri wako.

Rafiki,pamoja na majukumu ya lazima katika maisha yako ya kujenga nyumba,kuzaa watoto,kununua gari,bado unahitaji kutimiza ndoto kuu ya maisha. Ni kusudi la maisha yako. Ndiyo utambulisho wako duniani. Ni alama yako. Sasa swali,ndoto yako kuu ni nini duniani?

Ndoto kuu ya maisha ni jumla ya maisha yako yote. Anza kufikiria kuhusu ndoto yako kuu na uanze kuifanyia kazi. Kumbuka,kutimiza ndoto kuu hakuna muda maalum. Hujachelewa na wala hujawahi. Kama bado unaishi,una nafasi ya kutimiza ndoto yako. ” Ndoto kuu ya maisha ni jumla ya maisha yako yote”!

Hata hivyo,kutimiza ndoto kuu,itakubidi ulipe gharama yake!. Si kazi nyepesi,lazima ujitoe na ukubali kusonga mbele,pamoja na changamoto zote hizo, lazima utimize.
Thanks Numbisa.
 
je wewe una nini ambacho litakuwa historia kwa watoto wako na vizazi vyako .? Usilie maisha magumu huna mtaji anza na kile ulicho nacho mkononi mwako usiishie kutamani bali tengeneza mfereji wa pesa utazipata ukiamua kuishi wewe siyo mwingine.
Aliyenacho ataongezewa, asiyenacho hata kile alichonacho atanyanganywa.
 
Back
Top Bottom