Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Orania, ni mji unaopatikana Kaskazini mwa Afrika Ya Kusini. Wanaishi wazungu (Afrikaners) tu, wana Rais wao, fedha (Ora) na redio yao (Radio Orania). Mtu kutoka eneo lingine haruhusiwi kufanya kazi huko labda tu kama una ujuzi ambao hakuna mkazi wa huko anao.
 
Fredie Blom kutoka Afrika Ya Kusini ana miaka 116, ni moja kati ya watu wachache Duniani waliobakia kuwa na umri mkubwa zaidi kwa mujibu wa utafiti ambao ulionesha kuendana sawa na umri wake. Fredie anasema yupo hai mpaka sasa yote sababu ya mapenzi ya Mungu.
 
Kabila la Satere Mawe, Brazil mtoto wa kiume anapotimiza umri wa miaka 13, huonekana amekuwa mwanaume kamili kwa kuweka mikono yake sehemu maalum iliyowekwa siafu ambapo inabidi avumilie si chini ya dakika 5. Wengine hufanya hivyo zaidi ya mara 20 ili kupata sifa na kuaminika kama kijana aliyekomaa zaidi.
Soma zaidi Chanzo: Sites Google
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…