Ukiangalia marais karibu wote Afrika kusini mwa Jangwa la Sahara walibeba vifimbo.
Siku moja, wakati huooo, nikiwa kwenye kijiwe furani cha watu wazima nilisikia simulizi ya kuwa mti wa mpingo ni zindiko (Kinga) yenye nguvu ya kipekee.
Kwamba ukishika au kuweka mfukoni kipande cha mti huo unakuwa salama dhidi ya vitisho vyote.
Ukweli wa jambo hili wanaujua viongozi hao.
Hata hivyo kwa vyovyote vile, viongozi hawa wameshika fimbo hizo baada ya kupata maelekezo toka kwa washauri wao kwa sababu furani.