Numbisa
JF-Expert Member
- Dec 12, 2016
- 348,970
- 1,252,247
Rais wa Marekani donald trump amesema kuwa ikitokea akashindwa katika Kura za Uchaguzi wa Urais Mwaka huu dhidi ya Joe Biden , atafikiria kuihama nchi hiyo . Trump ameyasema hayo katika Moja ya mkutano wake wa Kampeni za Urais , na kusisitiza kuwa itakuwa ni fedheha sana kwake kushindwa dhidi ya Mwanasiasa mbovu katika hitoria ya nchi hiyo (akimaanisha Joe Biden) . "Mnajua kuwa Nina Presha sana kwasababu nagombea dhidi ya Mwanasiasi mbovu katika historia ya nchi hii , hivyo nikishindwa itakuwa ni aibu sana katika maisha yangu . Ikiwezekana naweza nikahama kabisa na nchi " - amesema Rais Trump