Asante sana ndugu yangu. Maneno ya hekima mno. Ndiyo. Binadamu huwa tunajisahaulisha mpaka tunafikia hatua ya kutendeana ubaya na hata kuuana. Lakini ukiyaangalia maisha kwa upana wake, unaweza ukakosa hata maana yake halisi. Mungu Atupe neema zake na Atupe maarifa na uwezo wa kuwa karibu naye na kutenda yale yanayompendeza. Muda wetu ni mfupi sana [emoji1545][emoji1545][emoji1545]
Hakika, maisha yetu ni mafupi sana. Muhimu tuwe watu wa kusaidia wenye uhitaji hata kwa msaada wa mawazo tu.
Hapa kituoni kwangu,kuna mtoto mwenye changamoto ya mwili (mlemavu) huwa anapenda kuja sana vile kuna ofisi nyingi maeneo haya.
Kiukweli ni mtoto ambae huwa ananiumiza sana nikimuona, sina uwezo mkubwa kifedha ila huwa nampa sana refreshments kama soda, biscuits au maji. Nikimpa yule mtoto huwa anafurahi sana, na akifurahi basi na mm huwa napata amani sana moyoni.
Huwezi amani wkend huwa natumia muda mwingi sana kumuwaza yeye kuliko hata watoto wangu, lakini jioni hii nimepata habari njema kuwa yule mtoto anahudumiwa sana na Plan international pamoja ma Help Age International.
Mara nyingi kama mzazi naumia sana nafikiria mtoto yule anatembea peke yake na hali yake ile, je usalama wake uko wapi?
So mara nyingi namsaidia, hata nikimkuta barabarani siwezi kuendelea na safari hadi nimtoe japo naumia sana.
Mazingira yangu ya kazi ni magumu mno kwa mtu alie na huruma kama mimi. Huwa nikirudi kwangu, nikikumbuka nalia sana kwa uchungu.