Kufanya upasuaji au kutumia dawa za kuongeza maumbile kama makalio huongeza hatari ya kifo cha mapema. Tambua mazoezi yanayoweza kukusaidia kutengeneza umbo zuri!
Unaweza kutibu tatizo la kukosa hamu ya tendo la ndoa kwa kufanya mazoezi mara kwa mara. Mazoezi huongeza stamina, hupunguza uzito, humfanya mtu kuwa na umbile zuri, furaha & kuongeza ufanisi wakati wa tendo la ndoa
Baadhi ya tafiti zimedai kufanya mazoezi alfajiri kabla hujala chochote husaidia mwili kupunguza uzito kwa haraka na kuufanya mwili kuwa na nguvu kwa siku nzima.
Ikiwa haupungui unene/uzito ingawa unafanya mazoezi basi jua unafanya mazoezi yasiyostahili mfano cardio kwa muda mrefu bila kubadilisha. Kufanya mazoezi haya kwa zaidi ya dakika 90 husababisha kuliwa kwa misuli muhimu inayoongeza kasi ya umetabol
Zoezi la kukimbia linaweza kumsaidia mtu kuondoa sonona/huzuni kubwa (depression) na wasiwasi (anxiety). Kwa vile mtu anapochangamka anafanya ubongo kutoa homoni ya furaha kwa wingi.
Kulingana na watafiti, mazoezi yakifanywa vizuri ni dawa bora ya kutibu maradhi mbalimbali mfano wanawake wanaopata maumivu makali wakati wa hedhi wakifanya mazoezi hupunguza maumivu
Ingawa kahawa huchochea maisha marefu na kupunguza hatari ya maradhi ya moyo na kisukari ila unywaji kahawa uliopitiliza unaweza kuashiria tatizo la sonona (mild depression) kitu kinachomfanya mtu kutegemea kahawa ili kutimiza baadhi ya majukumu yake
Kuamka mapema kabla ya kwenda kwenye shughuli zako husaidia mtu kujiandaa vizuri na kuwahi kwani kuchelewa kuamka humfanya mtu kuwa na wasiwasi mwingi hivyo kufanya viwango vya homoni ya mkazo (stress) kuongezeka sana
Vile umri unaongezeka ndio mifupa inavyodhoofu. Mifupa inapodhoofu inakuwa rahisi kuvunjika. Tafiti zimedai kukimbia kila siku kwa dakika 1-2 husaidia kuimarisha mifupa hasa ya nyonga.
Watoto kucheza nje na wenzao huwasaidia kuchangamsha miili yao, kupunguza hatari ya unene, kuimarisha mahusiano mazuri na wengine. Pia, husaidia watoto kutopata matizo ya macho hasa kutoona vitu vilivyo mbali, kulingana na utafiti wa hivi karibuni.
Ikiwa unapata shida kupata usingizi, wataalamu wa usingizi wanashauri kutotumia vifaa vya elektroniki masaa mawili kabla ya kulala, hasa ukiwa kitandani kitu kinachofanya ubongo uhisi kitandani ni mahala pa kazi na sio pa kulala
Kunywa maji kabla ya mlo husaidia kujaza tumbo na kumfanya mtu kutokula sana hivyo kumsaidia mtu kupunguza uzito au kuendelea kuwa na uzito unaofaa kiafya